Jumia inakuletea Vivutio vya Utalii Jijini Dar es Salaam... #share

Na Jumia Travel Tanzania
Umaarufu wa Dar es Salaam kwenye shughuli
za kibiashara umelifanya jiji hili kuwa vigumu kwa watu kuvizingatia
vivutio vyake vya kitalii. Watu wengi huvifahamu kwa kuviona tu lakini bila
ya kujua kihistoria sehemu hizo zina maana sana na wageni huja wakitokea
nchi mbalimbali kujifunza.
Ukiachana na ufukwe wa Coco Beach
unaopatikana pembezeni mwa bahari ya hindi eneo la Oyster Bay, Jumia Travel
ingependa kukufahamisha kwamba unaweza kujifunza na kufurahia mambo mengi
pindi utakapotembelea maeneo yafuatayo.
Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni.
Makumbusho haya awali yalifunguliwa mwaka 1940 kama kumbukumbu ya Mfalme
George wa tano ambapo kihistoria huwarudisha watanzania nyuma walipotokea.
Makumbusho haya huonyesha mabaki muhimu ya binadamu wa kale yaliyogunduliwa
na Dkt. Leakey aliyoyachimbua kwenye bonde la Olduvai. Wageni wanaweza
kujifunza urithi wa kitamaduni kutoka kwa makabila mbalimbali Tanzania
pamoja na athari za biashara ya utumwa kipindi cha utawala wa kikoloni.
Baadhi ya vitu vingine vinavyopatikana katika makumbusho haya yaliyopo mtaa
wa Shaaban Roberts ni zana za jadi, desturi, mapambo na vyombo vya muziki.
Kijiji cha Makumbusho. Takribani maili 6
kutokea katikati ya jiji, kuna kiji cha makumbusho ambacho kimehifadhi
tamaduni za makabila zaidi ya 120 yanayopatikana Tanzania. Wageni wanaweza
kuzunguka kwenye vibanda kadhaa vya nyasi vinavyopatikana pale kwenye ukbwa
wa takribani hekari 15 na kujionea ufundi wa kijadi katika kuchora, ufumaji
na uchongaji. Kijiji hiki kinachopatikana eneo la Kijitonyama, barabara ya
Bagamoyo pia huwa na ngoma na michezo ya jadi pamoja shughuli nyingize za
kitamaduni.
Sanamu la Askari. Likiwa limetengenezwa kwa
shaba sanamu hili ya Askari huonyesha askari akiwa amevalia vazi rasmi
lililotumika kipindi cha vita ya Kwanza ya Dunia huku ncha ya mbele ya
bunduki (kama kisu) ikiwa imeelekezwa karibu na bandari iliyopo jirani.
Sanamu hili huonyesha kama kumbukumbu ya majeshi ya waafrika walioshiriki
kupigana kwenye vita ya Kwanza ya Dunia na linapatikana mtaa wa Azikiwe na
Samora.
No comments:
Post a Comment