Makamu Samia alivyobariki 'arobaini' cha Makokoro Mwanza !
Maelfu ya nyavu aina ya kokoro zinazotumika kutekeleza uvuvi haramu Jijini Mwanza na vitongoji vyake leo yalitimiza 'arobaini' yake baada ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza zoezi la kuteketeza jumla ya nyavu 5662 za uvuvi haramu katika Dampo la Buhongwa.
Amesema amesema Mungu amewawekea ziwa wakazi wa maeneo hayo kwa makusudio yake, na Serikali haitavumilia kwa namna yoyote ile uharibifu wa rasilimali za ziwa hilo na kuwataka kulitunza.
Akiongea mara baada ya kukamilisha awamu ya kwanza ya zoezi hilo, Mama Samia amewataka viongozi wa Mkoa huo na Mikoa jirani kushirikiana na kuwachukulia hatua kali wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Amesema amesema Mungu amewawekea ziwa wakazi wa maeneo hayo kwa makusudio yake, na Serikali haitavumilia kwa namna yoyote ile uharibifu wa rasilimali za ziwa hilo na kuwataka kulitunza.
No comments:
Post a Comment