Matukio Pichani: Ziara ya Kimafunzo ya Maafisa wa Polisi Kutoka Chuo cha Ulinzi Rwanda.. #share




Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na mkuu wa chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda Kamishina wa Polisi wa Rwanda Felix Namhoranye ofisini kwake makao makuu ya Jeshi la Polisi. Kamishina Namhoranye ni kiongozi wa msafara wa maafisa mbalimbali kutoka chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda ambao wapo nchini kwa ziara ya mafunzo. Picha na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi.




Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na maofisa wa polisi kutoka nchi mbalimbali za Afrika mashariki na Afrika magharibi ambapo wanasoma chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda hawapo picha. Kushoto ni mkuu wa chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda, Kamishina Felix Namhoranye na kulia ni Kamishina wa Polisi Jamii , Mussa Alli Mussa – picha na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi.




Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Polisi kutoka nchi mbalimbali wanaosoma chuo cha ulinzi wa taifa cha Rwanda. Ujumbe huo unaohusisha maofisa wa Polisi kutoka nchi za Afarika mashariki na Afrika magharibi unaongozwa na Kamishina wa Polisi wa Rwanda Felix Namhoranye ambaye ndiye mkuu wa chuo cha ulinzi cha ulinzi cha Rwanda wapo nchini Tanzania kwa ziara ya kijifunza namna taasisi mbalimbali zinavyoendeshwa hapa Tanzania. Picha Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi.



Baadhi ya maafisa wa Polisi kutoka nchi mbalimbali za afrika mashariki na magharibi wanaosoma chuo cha ulinzi wa taifa cha Rwanda wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Tanzania makao makuu ya Jeshi la ( hayupo picha )wakati wa ziara yao ya mafunzo hapa nchini. Picha na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi.




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search