Video: Profesa Mbarawa 'afunguka' gharama zilizotumika kujenga MV Kazi,.. #SHARE

..aisifia 'Songoro Marine' kwa Ubunifu,.. #SHARE.. vivuko zaidi kujengwa kukabili changamoto ya usafiri !!

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi imeahidi kuendelea kutafuta njia mbalimbali kukabiliana na changamoto ya usafiri hasa katika maeneo yanayotegemea vivuko. 

Hayo yamesemwa leo na Waziri mwenye dhamana hiyo Profesa Makame Mbarawa wakati akipokea kwa niaba ya serikali kivuko kipya kinachofahamika kama MV Kazi. Kivuko hicho kitakachofanya safari kati ya Feri na Kigamboni ujenzi wake umegharimu Sh7.3 bilioni na kina uwezo wa kubeba watu 800 na magari 22 kwa wakati mmoja. 

Profesa Mbarawa amesema kivuko hicho kinakwenda kusaidia changamoto ya usafiri kwa wakazi wa Kigamboni ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia ufanisi mbovu wa vivuko vilivyopo.
 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search