Picha 21: Ujangili sasa basi.. TAWA wasema wamejipanga kupambana kwa kutoa mafunzo ya Kijeshi #SHARE
Katibu Mkuu akiwa pamoja na wahitimu Askari wanyamapori |
Mamlaka ya Wanyamapori imeanza
kazi rasmi tarehe 1/Julai/2016. Makao makuu yake kwa sasa yapo Morogoro katika
jengo la Taasisi ya utafiti wa mazao ya misitu (TAFORI). Majukumu ya TAWA ni
kusimamia na kulinda wanyamapori wote waliyopo maeneo ya nje za Hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongororo.
Wizara ya
Maliasili kupitia Mamlaka ya Usimamizi
wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imetoa mafunzo ya kijeshi ya kukabiliana na
Ujangili wa wanyamapori kwa Askari wanyamapori wapatao 75 kutoka katika Mapori
ya Akiba Rungwa, Ugala na vikosi Dhidi ya ujangili vya Manyoni na Arusha.Mafunzo
hayo yalifanyika katika Pori la Akiba
Rungwa/Muhesi/Kizigo, yakiendeshwa na askari wa jeshi la Marekani. Mgeni rasmi
alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mej.Generali Gaudence S.
Milanzi akifuatana na Mkurugenzi Mkuu wa
TAWA Bw. Martin Laibooki, Mkurugenzi
uzuiaji ujangili wa TAWA Bw. Faustin Masalu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
wanyamapori Bw. Canisius Karamaga, muwakilishi wa ubalozi wa Marekani ambaye ni
Mwambata wa jeshi la Marekani hapa nchini Tanzania Liutenat Colonel Michael
Lee, na wawakilishi wa mashirika ya wafadhili wa mafunzo hayo wawili kutoka
mashirika tofauti, Bw. Aaron Nicholas toka Shirika la ‘ Wildlife Conseration
Society- WCS) na Bw. Trevor Johnes toka shirika la uhifadhi la ‘STEP’. Aidha kulikuwa na wawakilishi wengine kutoka
mkoa wa Singida wakiwepo muwakilishi wa
RC na RPC.
Katibu Mkuu Mej.General. Gaudence Milanzi akisalimia na mwambata wa jeshi la Marekani nchini Tanzania Liutenant Colonel Micheel Lee kwenye Pori la Rungwa |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja
Jenerali Gaudence S. Milanzi amewataka wahitimu wa mafunzo hayo waliyopata kukabiliana na vitendo vya ujangili
kwa kuwakamata majangili na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
alitoa nasaha hizo wakati akifunga mafunzo ya watumishi wa wizara , Aidha alishuhudia mafunzo ya vitendo yalitoendeshwa kwenye makao makuu ya Pori la Rungwa kama picha hapo chini zinavyoonyesha.
alitoa nasaha hizo wakati akifunga mafunzo ya watumishi wa wizara , Aidha alishuhudia mafunzo ya vitendo yalitoendeshwa kwenye makao makuu ya Pori la Rungwa kama picha hapo chini zinavyoonyesha.
(Pichani nne Juu) Afisa wanyamapori Bw.Baraka Baragae akielezea vitendo vya mafunzo
vinavyoendelea hapo chini na jangili amekamatwa
Doria inaendelea na hatimaye jangili amekamatwa na kujeruhiwa baada ya mashambulizi makali na kubebwa
kusudi apate huduma ya kwanza
KATIBU MKUU AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WAHITIMU |
WAHITIMU WA MAFUNZO WANASOMA RISALA KWA MGENI RASMI WAKISHUHUDIWA NA MC |
Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Bw. Loibooki M. Akiwasikiliza wahitimu maoni yao |
Picha ya pamoja kati ya Katibu Mkuu na Walimu wa mafuzo hayo kutoka Marekani waliyochuchuma |
Mafunzo hayo yalianza Machi 27 hadi Juni 5, mwaka huu 2017 kwa maofisa 75 . Mafunzo waliyojifunza yalijikita kwa masomo yafuatayo; Upelelezi, Huduma ya kwanza,mbinu za kufanya doria, mazoezi ya viungo,usomaji wa ramani, GPS, ushirikishaji jamii katika uhifadhi na matumizi ya siraha.
Katika kushirikiana na Serikali ya Marekani kupitia
mashirika ya WCS na STEP wamesaidia
vifaa mbalimbali katika Mapori ya Akiba ya Rungwa/Muhesi/Kizigo vifaa
hivyo ni pamoja na magari manne, tractors 2, mafuta ya magari.
Katibu Mkuu akionyeshwa baadhi ya magari aina ya L/Cruiser yaliyonunuliwa na Serikali ya Marekani. Kushoto kwake anashuhudia Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Bw. Martin Loibooki |
Katibu Mkuu aliwaeleza wahitimu kuwa,yeye
binafsi natambua kuwa mafunzo haya hayakuwa rahisi kwenu haswa ukizingatia
wengi wenu kama siyo wote, hii ndiyo mara yenu ya kwanza kupata mafunzo kama
haya,lakini kwa dhamira nzuri na yenye mtazamo chanya mliyokuwa nayo imepelekea
wote kumaliza salama. Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatasaidia
kuimarisha nidhamu kwenye maeneo yetu ya
kazi katika kipindi hiki tunachojianda kuingia katika mfumo wa kiutendaji wa
jeshi usu.
Katibu Mkuu aliwaeleza wahitimu
kuwa Wizara inatambua mchango wa TAWA tangu kuanzishwa katika kukabiliana na
ujangili. Kuanzia mwezi Julai 2016 jumla ya majangili 3,185 wamekamatwa, kati
ya hao 1539 wamefikishwa mahakamani, na
siraha 270 na risasi 1058 zimekamatwa. Aidha askari wametegua mitego 3,273 ya
kuua wanyamapori. Nawapongeza sana TAWA.
Alimalizia hotuba yake kwa kuipongeza Serikali
ya Marekani na Mashirika yasiyo ya kiserikali ya WCS na STEP kwa mchango wake
katika uhifadhi.
Katibu Mkuu akisalimiana na Mratibu wa shirika la STEP Bw.Travor Johnes |
Katibu Mkuu akisalimiana na Mratibu wa Shirika la WCS Bw. Aaron Nicholaus |
KATIBU MKUU AKISALIMIANA MA MKUFUNZI WA MGAMBO WILAYA YA MANYONI BW. Lala Awe Silago |
Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Bw.Martin
Loibooki alimueleza mgeni rasmi kuwa Katibu lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwajengea
uwezo wa kuongoza watumishi walio chini yao ambao wengi ni askari.wakati
wahitimu hawa wengi wao hawajapata mafunzo ya kijeshi tangu wamalize elimu yao
ya chuo kikuu. Bw.loibooki alisema majukumu waliyopewa ni makubwa ambayo lengo
lake ni kuwaanda kuwa wahifadhi wakuu na baadaye. Hivyo ni vyema wakatambua
kuwa baada ya mafunzo haya wanajukumu yanawasubiri mbele yao.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Bw. Martin T.Loibooki,
alianza hotuba yake kwa kumshukuru Katibu Mkuu kukubali kuja kufunga mafunzo
hayo ya Maafisa wanyampori
Bw.loibooki alielezea kidogo
Mamlaka anayoisimamia kwa kuanza kusema, Mamlaka ilianzishwa na Serikali kama
chombo cha utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa niaba ya Serikali chini ya
uangalizi wa Serikali na kuwa na mfumo
unaonesha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi zaidi. Kama ilivyo kwa Mamlaka
Serikali nyingine nchini, lengo la kuanzishwa TAWA ni kutekeleza majukumu ya
Idara ya Wanyamapori hasa ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini. Majukumu ya TAWA ni kusimamia shughuli za utawala, ulinzi,
usimamizi wa raslimali ya Wanyamapori katika maeneo yote nje ya Hifdahi za
Taifa na Hifadhi ya Ngorongoro.
Akiitimisha hotuba yake Bw.
Loibooki alizungumzia suala la ujangili kwa kusema, TAWA inaamini kwamba
changamomoto za ujangili na uvunaji haramu wa misitu na matatizo mbalimbali
yanayohikabili uhifadhi nchini hayawezi kutatuliwa kwa mfumo wa utendaji kazi
wa kiraia. Hivyo, Wizara inakamilisha taratibu za kubadili mfumo wa utendaji
kazi kutoka wa kiraia kwenda jeshi usu.Mabadiliko haya ya kimfumo ni matakwa ya
Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009 ambayo imeanisha kwamba
kutaundwa kikosi cha jeshi usu (Wildlife
Protection Unit), ili kuhakikisha ulinzi kamili wa rasilimali katika maeneo
yaliyohifadhiwa
BW.MARTIN T. LOIBOOKI (KAIMU MKURUGENZI MKUU |
Bw. Loibooki alimueleza mgeni rasmi anawashukuru
Serikali ya Marekani kupitia shirika lisilo la Kiserikali la WCS kwa kutoa
mafunzo ya kikosi maalumu cha kukabiliana na ujangili kwa haraka zaidi
kiitwacho ‘Rapid Response Team’ ambacho kimepatiwa vifaa ikiwepo magari ya
doria kwenye Mapori ya Akiba ya Rungwa, Rukwa na Piti. WCS vilevile wanasaidia
doria ya kutumia ndege katika kukabiliana na ujangili.Hapo chini ni baadhi ya
kikosi hicho.
Mkurugenzi Mkuu akimuelezea mgeni rasmi utendaji kazi wa kikosi hicho cha ‘Rapid Response Team’ kinavyofnya kazi |
AFISA HABARI NA MAHUSIANO WA TAWA BW.TWAHA TWAIBU AIKWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KIKOSI CHA ‘RAPID RESPONSE TEAM’ RUNGWA |
KAIMU MKURUGENZI MKUU BW.LOIBOOKI AKITELEMKA KWENYE UWANJA WA RUNGWA AMEFUATANA NA KATIBU MKUU |
No comments:
Post a Comment