Siasa za Upinzani zina Mambo; Hebu ona hapa Uhuru Kenyatta 'alivyomsubirisha' Raila Jukwaani!!

Maadhimisho ya Miaka 54 ya Sikukuu ya Madaraka Day Nchini Kenya leo yalikuwa Machungu kwa Mwanasiasa Mkongwe mwenye 'Heshima zake' Raila Odinga baada ya waandaaji wa Sikukuu hiyo ya Kitaifa kuamua 'kumpotezea mazima'.
Licha ya kuacha ratiba yake ngumu ya kampeni zinazoendelea na kuwahi eneo la tukio kulikofanyika Maadhimisho hayo Mjini Nyeri, na kuhudhuriwa na maelfu ya Wananchi na wageni mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa Nchi Wafadhili, Raila ambae pia ni Mgombea Uraisi Wa Jubilee kupitia Muungano wa NASA, aliendelea kubaki na shauku mda wote wakati wageni waalikwa na Viongozi wakitambulishwa lakini jina lake halikuwepo kabisa kwenye Ordha.
Hali ilizidi kuzua taharuki kwake na wafuasi wake wakati Gavana wa Nyeri alipomuita Makamo wa Rais William Ruto kumkaribisha Rais alihutubie Taifa kuashiria kuhitimisha sherehe hizo, jambo lililomfanya Raila kuondoka kimya kimya kama aliemwagiwa maji!
Maelfu ya watumiaji wa social media walifurika mtandaoni kumpa pole Raila na kulaani kitendo cha waandaaji na kukiita si cha kiungwana hata kidogo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search