Simbachwene: waliochaguliwa kidato cha tano, vyuo.. hawa hapa, wasioripoti ndani ya wiki mbili kupigwa mkasi !!

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.
Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.
Alisema kwa taasisi ya watu wazima waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ni 21 tu.
Alisema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama vilivyoaibishwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.
Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.
"Na kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," alisema Simbachawene.
Mbali na hilo amewaagiza wakuu wote wa mikoa na wakuu wa wilaya kukamilisha ujenzi wa madarasa na mabweni kwenye shule zote ambazo zinahitajika kuwapokea wanafunzi wa kidato cha tano ili shule zitakapofunguliwa wanafunzi waanze masomo Mara moja.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search