Business News: Sikukuu ya Idd el-Ftr Yashusha Mauzo ya Soko la Hisa (DSE).. #share
SIKUKUU ya Idd el-Fitr imetajwa kuwa chanzo cha kushuka kwa asilimia 98, mauzo ya hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa wiki iliyoishia June 30 mwaka huu.
Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Afisa Mwandamizi wa Masoko ya DSE Mary Kinabo akizungumza na waandishi wa habari akito taarifa mauzo ya hisa ya mauzo ya hisa kwa wiki iliyopita.
Alisema idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepungua kutoka hisa milioni 2.39 kwa wiki iiliyopita ya Juni 23 hadi kufikia hisa 335,000 Juni 30 mwaka huu ambapo alisema imechangiwa na siku mbili za sikukuu ya Idd el-Ftr.
“Hivyo pia thamani ya mauzo ya hisa kupungua kutoka shilingi bilioni 19 wiki iliyopita hadi shilingi milioni 412 wiki hii iliyoishia juni 30, 2017,” alisema Kinabo.
Alitaja kampuni zilizoongoza kwa mauzo ya hisa kuwa ni Kampuni za Sigara Tanzania (Tcc) asilimia 70.41, Banki ya CRDB asilimia 11.86 na Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) asilimia 7.97.
Aidha alisema ukubwa wa mtaji wa kampuni hizo zilizoorodheshwa umepanda kwa shilingi bilioni 438 kutoka sh. trilioni 18.8 wiki iliyopita hadi sh. trioni 19.3 wiki iliyoishia Juni 30 mwaka huu ambapo alibainisha kuwa hiyo inatokana na kupanda kwa bei za hisa za USL (15.38%), TCC (12.76%) na KA (7.14).
Alieleza kuwa ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa sh. trilioni 7.75 wiki hii kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za TCC (12.76).
Alifafanua kwamba mauzo ya hati fungani katika wiki hiyo ya Juni 30 yamepanda kutoka sh. milioni 770 wiki iliyopita hadi sh. bilioni 9.6 ambapo alisema mauzo hayo yalitokana na hatifungani nne za serikali na za makampuni zenye jumla ya thamani ya sh. bilioni 11.4 kwa jumla ya gharama y ash. bilioni 9.6.
Kinabo alisema kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 40 kutoka pointi 2,127 hadi pointi 2,166 kutokana na kuongezeka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.
Alisema kufuatia kupanda kwa bei za hisa, kiashiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 59 kutoka pointi 3,632 wiki iliyopita hadi pointi 3692 wiki hii.
Aidha alisema kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) imepanda kwa pointi 4,803 wiki iliyopita hadi pointi 4914 wiki hii kutokana na kupanda kwa bei za hisa za TCC kwa 12 .76% kutoka sh. 9,800 hadi sh. 11.050.
Aliongeza kwamba kiashiria cha huduma za kibenki na Fedha (BI) wiki hii kimepungua kwa pointi 0.6 kutoka pointi 2,515 hadi pointi 2,514.64 kutokana na ongezeko la bei ya hisa za DSE (1.69%) huku kiashiria cha sekta ya huduma za kibiashara (cs) wiki hii imebaki kwenye wastani wa 2,467.
Kwa upande mwingine Kinabo alisema shindano la DSE SCHOLAR INVESTMMENT CHALLENGE 2017 lilifika mwisho Juni 30 mwaka huu ambapo zaidi ya wanafunzi wa vyuo na sekondari 11,000 walishiriki katika shindano hilo ikiwa ni idadi zaidi ya mara tatu kwa mwaka uliopita.
Alisema matokeo ya washindi wa shindano hilo yatatangazwa Julai 10 zoezi la uchambuzi litakapoanza - Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment