News Flash: Halima Mdee aibukia 'Mimba Mashuleni..' Mama Samia ahudhuria AU Summit Addis #share.. Note 7 Yarudi Sokoni Kiaina..

Mdee ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wake aliofanyia makao makuu ya Chadema jijini hapa.
Amesema viongozi wa halmashauri hizo hawapaswi kuogopa kutimiza wajibu wao kutokana na kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia wanafunzi wanaopata mimba kutoendelea na masomo.
Alisema wenyeviti wa halmashauri zilizopo chini ya Chadema waonyeshe mfano kuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi Katiba na sheria ikiwamo ya elimu ambapo pamoja na mambo mengine inaweka misingi ya kupata elimu na kutobaguliwa kwa kigezo chochote.
"Nafahamu Rais anachukia wanawake, ana mfumo dume hii imeonyesha kwenye uteuzi wake, ila sikujua kama anawachukia hadi wasichana yaani msichana akipata mimba shule ndoto zake zinazimwa, wengine walibakwa,"alisema Mdee - Mcl digital 
































About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search