tRENDING nEWS: Madame Fatma Karume,.. 'amuamshia dude' aliemshika mwili wake'.. adai 1billion.. #share

Wakili wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Fatma Karume amefungua kesi ya madai Mahakama Kuu ya Tanzania dhdi ya Inspekta wa Polisi Eugene Mwampondela wa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es salaam.




Fatma amesema kuwa Inspekta Mwampondela alimshika mkono na kumvuta kwa nguvu hali iliyomsababishia maumivu makali, hivyo anadai alipwe kiasi cha shilingi bilioni moja kwa kosa la kumwingilia mwilini mwake na kumbughudhi kwa kumzuia kufanya kazi yake.

“Aliniambia kuwa ameagizwa na wakubwa kutoka juu, hivyo namfikisha mahakamani ili amweleze jaji ni nani aliyemtuma, na mimi sitaki kushikwa shikwa mwili wangu kwa hiyo naomba anilipe shilingi bilioni moja ili liwe fundisho kwa wengine,”amesema Fatma.

Hata hivyo, Fatma ambaye ni mmoja wa mawakili wa Mbunge wa SingidaMashariki alikumbana na kadhia hiyo wakati akiwa katika harakati za kumtetea mteja wake ili aweze kupata dhamana -D24

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search