eXCLUSIVE ya matukio360 na Hashim Rungwe kudai eti CUF 'inatafunwa na wenye njaa'.. atoa dira ya kuua mgogoro.. #share
MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma) Hashim Rungwe, amesema mgogoro unaoendelea
ndani ya Chama cha Wananch CUF ni kuwepo kwa kundi linaloangalia maslahi binfsi
ya matumbo yao.
Kauli hiyo Rungwe ameitoa leo wakati
akizungumza na Matukio360, amesema njaa ndiyo imeifikisha CUF katika sakata
hilo na kuonyesha kusikitishwa na jinsi chama hicho kikongwe nchini kwa sasa
kinavyokosa mwelekeo wa kisiasa.
“Mgogoro wa CUF wa sasa
unasababishwa na njaa, kwa maana ya kwamba kuna kundi, linachoangalia sana ni
maslahi ya matumbo yao, hawana ajenda yani ya maana ya kuleta mabadiliko,”
alisema Rungwe.
Aidha ameeleza kuwa kundi hilo
linapambana na kundi la pili ambalo limejidhatiti kwa ajili ya kuleta mabadiliko
ya kweli na kutotanguliza njaa.
Amebanisha kuwa kundi hilo la pili
kama lingekuwa na maslahi binafsi lingekuwa limetulia kwani fursa ilikuwa ya
kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar lakini limekataa na kusema kuwa linataka
kuendelea na mapambano ya kubadilisha mfumo uliopo katika serikali.
Rungwe ameonyesha masikitiko juu ya
sakata hilo na kusema ni bahati mbaya kwa kuwepo kwa pande hizo mbili ambazo
zinasigana. Alibainisha kuwa katika pande hizo kuna upande ambao umeonyesha
kuungwa mkono na watu wenge huku mwingine ukiungwa na wachache.
Kutokana na hali hiyo ameshauri
wanaodhani kutotendewa haki kwa sababu ya sakata hilo akitolea mfano wabunge
waliovuliwa uanachama kwenda mahakamani kwani ndiyo mahali pekee wanapoweza
pata haki yao.
Na: Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment