tETESI zA uSAJILI bARANI uLAYA: Usajili wa Neymar kwenda PSG wamvuruga kichwa Valverde wa Barcelona #share..
Kocha wa Klabu ya Barcelona
Ernesto Valverde amesisitiza kuwa Neymar yupo katika mipango yake msimu ujao na
kukanusha tetesi za dili la mchezaji huyo kuhamia PSG kwa dau la £195m.
Kocha huyo aliulizwa
maswali kuhusu mipango yake juu ya mchezaji huyo wakati huu ambapo klabu ya Paris
St Germain's iko tayari kuvunja rekodi ya usajili kwa dau la £195m.
Amesema: 'Kila mara
najaribu kuzungumzia kuhusu masuala yanayotokea kuliko masuala ambayo yanayoweza
kutokea. Tunakwenda kusubiri. Kwa mtazamo wangu tunaye Neymar kwenye timu yetu,
tunamtegemea, tunapaswa kuona,” amesema.
“Sitaki kutafakari kuhusu Neymar. Ninamwona katika sehemu ile ile
ninayomuona hivi sasa – uwanjani na sisi,” amesisitiza.
Katika siku za hivi Neymar
da Silva Santos Júnior, (25) amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa kuhamia
klabu ya PSG ya nchini Ufaransa hadi jana taarifa zilikuwa zinadai kuwa ata
saini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo.
chanzo: Mail Online
No comments:
Post a Comment