Heka Heka.. Watoto wanne (4) waliopotea Mjini Zanzibar wapatikana kwenye gari wakiwa maiti.. #share

Siku ya Jana ya tarehe 16/07/2017, katika maeneo ya Jang'mbe Mjini zanzibar kulitokea mkasa wa kusikitisha wa watoto wanne wenye umri wa kati ya miaka 2 hadi minne ambao walitoweka machoni mwa wazazi wao na walezi wao kwa masaa kadhaa.



Baada ya bidii kubwa ya kuwatafauta watoto hao iliyowashirikisha wananchi ndugu jamaa na viongozi wa Jimbo la Jang'ome, 'hamad.. majira ya usiku watoto hao wote wakakutikana ndani ya gari wakiwa wameshafariki dunia..' Tumsikilize katibu wa Viongozi wa Jimbo la Jang'ombe Bw. Omar Abdallah Othman akielezea kwa kuktasari tuu mkasa mzima..

Bofya hapa chini...

"Ndugu zangu tumepatwa na Msiba mzito wa ndugu zetu watoto wadogo wa miaka 3 na 2 idadi yao ni wanne 4 ambao walipotea mchana wa 16/07/2017 na jitihada za kuwatafuta zilitumika bila mafanikio, na majira ya saa 2 ucku walikutikana katika gari moja iliyoegeshwa katika maeneo ya malazio ya magari wakiwa tayari wameshafariki Dunia. 

Viongozi wa Jimbo la Jang'ombe na wananchi waliungana katika harakat hizo na Inshaallah kesho maziko yatakuwa saa 7 msikiti wa Jang'ombe Mshelishelini ulipotokea mkasa wa kustaajabisha wa kuzama Nyumba... Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema pepon Amiiiiin..."

Bw. Omar akamalizia kwa kusema "Maziko yatakuwa ni kwa pamoja ingawa kila mmoja ana nyumba yao na wazazi wake ila kama viongozi tumezungumza na familiar zote na kukubaliana kufanyika maziko ya pamoja ili wananchi wote wapate kushiriki..." INNA LILLAH WA INNA ILAYHI RAAJ'UUN...




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search