Kimataifa News: Serikali ya Uingereza Kutumia Qatar Airways kukabili mgomo British Airways.. #share huku saudi ikiitisha Vikwazo zaidi

Serikali ya Uingereza imesema haitajali vikwazo vilivyoekewa Nchi ya Qatar na mataifa nduguze, na itatumia ndege za shirika la Qatar Airways kushika nafasi ya shirika la British Airways wakati wafanyakazi wa Shirika hilo kubwa la Ndege la Uingereza wanapoingia kwenye wa mgomo ulioanza leo; na unaotajiwa kudumu kwa muda wa wiki 2.

Maofisa wa mambo ya usafiri nchini Uingereza wamesema angalau ndege 9 kutoka Qatar zitaazimwa kukabiliana na mgomo huo unaohusu mambo ya maslahi ya malipo ya mishahara na posho kwa wafanyakazi.

Qatar inamiliki maslahi mapana katika shirika la British Airways, na nchi zote mbili ni sehemu ya wamiliki wa mashirika makuu ya OneWorld Alliance na Code Share na wamekuwa kwenye ubia wa muda mrefu wa uendeshaji mashirika hayo.

WAKATI HUO HUO: Saudi Arabia na nchi tatu za kiarabu zimeongeza muda kwa nchi ya Qatar, kutimiza masharti iliyopewa la sivyo iwekewe vikwazo zaidi baada ya saa 48.
Tarehe ya mwisho ya kuitaka Qatar kukubali masharti 13, ikiwemo ya kukifunga kituo cha Al Jazeera ilimalizika siku ya Jumapili.
Taifa hilo la ghuba linasema kuwa litajibu kupitia barua ambayo itawasilishwa kwa Kuwait leo Jumatatu.
Qatar inakana madai kutoka kwa majirani zake kuwa inafadhili itikadi kali.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini humo, atasafiri kuenda Kuwait leo, kuwasilisha barua hiyo iliyotumwa kutoka kwa emir wa Qatar kuenda kwa emir wa kuwait ambaye ndiye mpatanishi mkuu wa mzozo huo.
Siku ya Jumamosi waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani, alisema kuwa taifa hilo lilikataa masharti hayo lakini liko tayari kwa mazungumzo.
Qatar imekuwa chini na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa wiki kadha sasa, kuetoka Saudi Arabia, Misri, milki ya nchi za kiarabu na Bahrain.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search