Breaking News: Jamal Malinzi, Rwegamalila na Harbinder Singh.. 'mguu kwa mguu' Mahakamani,.. #share.. warudishwa 'mahabusu'

Mwenyekiti wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Celestine Mwesigwa wamepandishwa kizimbani kwa mara ya pili leo 03/07/2017 kusomewa mashtaka na kisha wamerudishwa mahabusu baada ya kukataliwa dhamana na watafikishwa tena Mahakamani tarehe 17/07/2017.

Wawili hao wanakabiliwa na mashitaka mbalimbali kuanzia 25 hadi 28 likiwemo lile la matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji wa fedha.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri  alisema upande wa utetezi wenyewe wanatambua kuwa mashitaka ya utakatishaji fedha hayana dhamana.



Wakati huo huo,..  Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engeneering na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira na Habinder Seth Sigh, Mwenyekiti Mtendaji wa PAP wamefikishwa mahakamani leo na kuongezewa mashtaka mengine sita ya kuhujumu uchumi.








Awali watuhumiwa hao walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma ya uhujumu uchumi na kula njama, kughushi, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababisha hasara serikali, lakini watuhumiwa hao leo tena wamepandishwa kizimbani na kuongezewa makosa mengine sita ya ya utakatishaji wa fedha na kufikisha jumla ya mashtaka 12.
Mbali na hilo watuhumiwa hao wamekwama baada ya kukosa dhamana tena na wote wamerudishwa rumande mpaka tarehe 14 Juni mwaka huu ambapo kesi yao itasomwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. 




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search