News Flash !! JPM Ataka muda Uongezwe '77; atembelea banda la LHRC.. #share Trump asema 'tumewachoka Korea..' Eti kwa nini huwezi acha kula chipsi..? haya soma hapa..!

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe MagufulI ameiagiza mamlaka ya maendeleo ya biashara -TANTRADE  kuongeza muda wa maonesho ya biashara katika viwanja vya sabasaba ili watanzania waendelee kutembelea na kujifunza teknolojia zinazooneshwa.

Akiongea kwenye ufunguzi wa maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa Dar es salaam yanayofanyika katika uwanja wa maonesho ya biashara wa Mwalimu Nyerere yaliyopangwa akudumu hadi July nane Rais MAGUFULI amesema mamlaka  haitapoteza chochote ikiongeza muda ili watanzania wafike kwa wakatiwao kujifunza na kununua bidhaa.
Aidha rais amezuia azma ya mamlaka hiyo kujenga hoteli ya kimataifa ndani ya uwanja huo na badala yake ameagiza wajenge viwanda vya mfano.
Maonesho ya mwaka huu yameshirikisha nchi 26 na yana kauli mbiu ya "ukuzaji wa biashara kwa maendeleo ya viwanda" ambapo makundi mbalimbali yalioyoshiriki kutoka ndani na nje ya nchi yamezawadiwa ambapo Ujerumani imeibuka mshindi wa kwanza kwa washiriki kutoka nje waliofanya vizuri zaidi na Mshindi wa jumla ni chuo kikuu cha Dare s Salaam - Redio One !


=========    ========    ======

HUKO MAREKANI NAKO: Rais wa Marekani Donald Trump anasema muda wa uvumilivu wa kimikakati kwa Korea Kaskazini umekamilika sasa. Katika hotuba ya pamoja na rais wa Korea Kusini Moon Jae, kwenye ikulu ya White house, Trump amesema kwamba vitisho vya Korea Kaskazini vinafaa kupata majibu ya kijasiri. Hata hivyo, Trump amesema ni muhimu kuwe na ushirikiano katika kugawana mzigo wa kuhakikisha usalama. Rais wa Korea Kusini amesema kwamba taifa lake litaweka marekebisho ya kiuslama na kujenga msingi dhabiti wa kujikinga. Rais Moon pia amesema ni muhimu kuendelea na majadiliano na viongozi wa Korea Kaskazini.










About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search