Press Release: Baada ya wiki iliyopita thamani ya mauzo ya hisa kuongezeka mara 15, Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Leo wametuletea hii... #share.
THAMANI ya mauzo ya hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa wiki hii imepungua kwa asilimia 36 kutoka sh. bilioni 6 wiki iliyopita hadi sh. bilioni 3.9 wiki hii iliyoishia Julai 14 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mwandamizi wa Masoko DSE Mary Kinabo akizungumza na waandishi wa habari, hata hivyo alisema idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kwa 26% kutoka hisa 13.6 wiki iliyoisha Julai 6 hadi hisa milioni 17 kwa wiki iliyoishia Julai 14.
“Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuaatavyo, Banki ya CRDB asilimia 89, TBL asilimia 8 na DSE asilimia 0.9,” alisema Kinabo.

Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Akizungumzia suala hilo amesema ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 516 kutoka Shilingi Trilioni 18.7 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 19.2 wiki iliyoishia Julai 14. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei za hisa za USL (34%), ACA (9%) na JHL (5%).
Aidha amefafanua kwamba ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 13.5 kutoka Shilingi Trilioni 7.70 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.72 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za CRDB (2.5%).
Hati Fungani (Bonds)
Kwa upande wa hati funganu ameeleza kuwa tofauti na ilivyokuwa kwenye hisa, mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia Julai 14 yamepanda kutoka Shilingi bilioni 12.25 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 44.3

Amesema mauzo hayo yalitokana na hatifungani kumi na saba (17) za serikali na za Makampuni binafsi (Corporate Bonds) zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 51 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 44.3.
Viashiria (Indices)
Amebainisha kwamba Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 59 kutoka pointi 2,151 hadi pointi 2,211 kutokana na kuongezeka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.

Kinabo amesema kufuatia kupanda kwa bei za hisa, kiashiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 6 kutoka pointi 3,666 wiki iliyopita hadi pointi 3673 wiki hii.
Aidha kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) imebaki kama awali kwenye wastani wa TZS 4809.
Kiasharia cha huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii kimepanda kwa pointi 17 kutoka pointi 2,598 hadi pointi 2,616 kutokana na ongezeko la bei ya hisa za CRDB (2.5%)
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kwenye wastani wa 2,467 kama awali.
Na Abraham Ntambara

No comments:
Post a Comment