sPORTS nEWS: Winga Emmanuel amaliza utata.. Okwi atua Sauz kwa pipa.. Kocha asema ni 'engine ya programu zetu'
Winga mwenye nguvu, kasi na akili nyingi awapo ndani ya 18, Emanuel Okwi raia wa Uganda aliesajiliwa na Simba SC toka SC Villa hivi karibuni amewasili nchini Afrika Kusini jana jioni kujiunga na wekundu hao wa msimbazi waliojichimbia nchini humo takribani wiki mbili sasa.
Emanuel Okwi anaeimudu vyema wing ya kushoto na kucheza kama kiungo mshambuliaji, alichelewa kujiunga na kambi hiyo kutokana na kusubiri tuzo za ligi kuu nchini Uganda kupita ambazo zilifanyika usiku wa alhamisi .
Katika tuzo hizo, Emanuel Okwi alikuwa kateuliwa katika kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa ligi hiyo inayodhaminiwa na Azam media sanjari na Geofrey Sserunkuma mshambuliaji wa Kampala City Council Authority (KCCA) ambaye aliibuka mchezaji bora kwa kumbwaga Emmanuel Okwi.
Kocha mkuu wa Simba SC amefurahi kuwasili kwa mchezaji huyo kambini ili wachezaji wote kuenenda vyema na programu zake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ngao ya jamii na watani zao Yanga SC August 23 na maandalizi ya ligi kuu kwa msimu mpya wa 2017-18.
Simba SC wameweka kambi katika jiji la Joharnesburg na kwa fununu zilizopo huenda leo jioni kiungo Haruna Niyonzima anaweza kujiunga na kambi hiyo . Haruna Niyonzima aliyewika na Yanga SC kwa zaidi ya misimu mitano inasemekana amemalizana na mabingwa hao wa kombe la ASFC 2016-17 na tayari ametumiwa nauli kutoka nchini kwao Rwanda ili kujiunga na kambi hiyo nchini Afrika Kusini kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya Tamasha la Simba day August 8, 2017.
Wakati huohuo jana jioni kikosi hicho kikiwa mazoezini, aliyekuwa beki wao wa kati Abdi Banda aliesajiliwa nchini humo na klabu ya Baroka aliwatembelea kuwasalimia na kuonesha bado anaithamini klabu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa imechangia maendeleo yake kisoka mpaka sasa.
Abdi Banda ameingia kandarasi ya miaka mitatu na Baroka FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo - soka360
No comments:
Post a Comment