TOP NEWS: Furaha ya JPM ikakamilika hapa..Mama Samia kaenda Addis.. Diamond Platnumz aendelea 'kuwamwaga machozi' Waganda.. #share CHADEMA yataka viongozi wenye 'uchu' wa kuhama waharakishe.. Trump uso kwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwasili Wilayani Sengerema kuzindua Mradi wa Maji ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2014 kwa gharama ya Sh23 bilioni utawanufaisha zaidi ya wakazi wa wilaya hiyo zaidi ya 13,000.

Mhandisi wa Maji Wilaya ya Sengerema, Nikas Ligombi alisema mradi huo uliofadhiliwa na Benki ya Afrika umekamilika kwa asilima 100 na utakapozinduliwa rasmi tatizo la maji katika mji wa Sengerema litakuwa limepatiwa ufumbuzi.
“Lita za ujazo 150,000 zitakuwa zinasukumwa kila siku kutoka kwenye chanzo cha maji kwenda kwenye matanki ya kusambaza mitaani,” alisema Ligombi.
Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema, Magesa Mafuru alisema ni fahari kubwa kukamlika kwa maradi huu ambao utamaliza matatizo ya maji yaliyokuwa yakiukabili mji huo na kuwataka wananchi kuutunza na kuuthamini ili udumu kwa muda mrefu.
Mmoja wa wakazi wa mjini humo, Jumanne Kashiba alisema baada ya mradi huu kukamilika tatizo la maji mjini hapo lilokuwa likiwakabili litakoma na kuipongeza serikali kwa jitihada hizo - Mwananchi Online..



Matukio tumekukusanyia 'Top news' zinazojiri Nchini penu mda huu vikiambatana na vionjo kadhaa vya Burudani.. 

Fuatana nasi kupitia uzi huu kila baada ya nusu saa, tutakujuza hatua kwa hatua..




























About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search