Top news: JPM Kuzindua Upanuzi wa Bandari Kesho; Picha za Staa Lionel Messi Alipopata jiko jana.. Ndugai nae 'motooo'.. #share Nkurunziza nae anena kwa 'kirundi'

Ndugu yangu msomaji, usipitwe na matukio muhimu yaliyojiri usiku wa kuamkia leo.. fuatana na matukio360 ikuhabarishe hatua kwa hatua..



Spika wa Bunge Mh Job Ndugai ametoa onyo kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakitumia lugha zisizofaa bungeni na kuliita bunge kuwa ni dhaifu.
Spika wa Bunge Mh Job Ndugai amesisitiza kuwachukulia hatua wabunge watakaokwenda kinyume na kanuni na taratibu za Bunge na kiti cha Spika likiwemo la kutumia lugha zisizo na staha katika Bunge.
Kamati ya pamoja ya Bunge inayojumuisha kamati za bunge nne yaani Kamati ya Madini,Kamati ya Katiba na sheria,Kamati ya sheria ndogo na kamati ya ardhi maliasili na mazingira imepokea taarifa ya miswada ya sheria mitatu ya mikataba ya rasilimali za nchi kutoka serikalini kupitia Waziri wa Katiba na sheria Prof Palamagamba Kabudi watakayoijadili na kuwasilisha bungeni baadae.
Miongoni mwa yatakayokuwamo katika miswada hiyo ni pamoja na kuboresha ushiriki na umiliki wa wananchi katika rasilimali za nchi lakini pia bunge kupewa nguvu ya kupitia mikataba ya madini kabla ya kusainiwa - ITV












About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search