bREAKING nEWS: Dkt. Abbas ajibu mapigo ya Mbowe kwa Takwimu.. #share

KATIKA kile kilichoelezwa Serikali kukijibu Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kuhusu hali ya uchumi nchini, Serikali imetoa takwimu zinazoonyesha
ukuaji wa uchumi katika sekta mbalimbali. 


Hatua hiyo imekuja baada ya Chadema kutoa taarifa inayoeleza hali ya uchumi wa nchi iko katika hali mbaya kwenye sekta mbalimbali.

Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa vyombo vya habari leo
jijini Dar es Salaam Msemaji Mkuu wa Serikali Hassan Abbasi alisema kwa mujibu wa
takwimu za Benki ya Dunia (BoT) na Shirika la fedha Duniani (IMF) zinaonyesha
uchumi wa dunia kwa ujumla ulipata matanziko ambapo kufikia Aprili mwaka 2016
ulikua kwa asilimia 3.1 ukilinganishwa na asilimia 3.5 mwaka 2015.

" Takwimu za BoT na hata Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), pamoja na mtikisiiko
huo duniani ambao umeathiri kidogo nchi nyingi ikiwemo Tanzania, zinautaja uchumi
wa Tanzania kuwa uko imara," alisema Abbasi.

Ababsi alisema uchumi wa nchi kwa miaka mitatu mfululizo hadi sasa bado uko katika
ukuaji usiopungua asilimia 7.0 hadi 7.2 ikiwa ni ukuaji wa juu katika ukanda huu
(Rwanda 6%, Uganda 5% na Kenya 6.4%).

Alisisitiza kuwa makusanyo yameongezeka kutoka wastani wa Sh bilioni 925 kwa
mwaka 2015 hadi Sh trilioni 1.609 kwa mwezi juni mwaka huu huku akiongeza
ongezeko hilo ni sawa na asilimia 15 kwa mwaka.

Aidha, alisema wakattio hali ya mfumuko wa bei ikiwa juu katika nchi mbalimbali za
Afrika takwimu za NBS za Juni mwaka huu zinaonyesha mfumuko wa bei wa Tanzania
umeshuka hadi asilimia 5.4 kutoka 6.1 ya mwezi Mei mwaka huu.

Alifafanua kuwa katika Ukanda wa Afrika kiwango cha mfumuko kilichowekwa
kinatakiwa kisisidi asimilia 8 na kwamba kwa mujibu wa Fahirisi ya Uwekezaji Afrika
iliyotolewa na Taasisi ya Quantum Global Research inaonyesha Tanzania ni nchi ya
kwanza kwenye ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuvutia wawekezaji na
ya nane barani Afrika ikipanda kutoka nafasi ya 19 mwaka 2015.

Abbasi alisema katika kipindi cha Julai mwaka jana hadi machi mwaka huu biashara
7,277 zilifungwa lakini katika kipindi hicho hicho biashara mpya 224,738 zilisajiliwa.

Katika hatua nyingine alisema katika sekta ya afya Serikali iliongeza bajeti kutoka Sh
bilioni 796 hadi Sh trilioni 1.077 kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Pia alisema bajet i ya dawa na vifaa tiba imeongezeka kutoka Sh bilioni 30 mwaka
2015/16 hadi Sh bilioni 251 mwaka 2016/17 ambapo bajeti ya sasa ni sh bilioni 261.

Abbas alisema kwenye sekta ya elimu Serikali imeendelea kutoa elimu bure kuanzia
darasa la kwanza hadi kidato cha nne kwa kutenga Sh bilioni 18 kila mwezi.

Wakati huo huo, alisema wakati Serikali inaingia madarakani mikopo ya elimu ya juu
ilikuwa Sh bilioni 341 lakini Rais aliongeza hadi Sh bilioni 475 na mwaka 2016/17
zilifika Sh bilioni 483 huku bajeti ya sasa zikitengwa sh bilioni 427.

Alisema sekta ya nishati uzalishaji wa umeme umeongezwa kwa kujenga Mradi wa
Kinyerezi I unaozalisha Megawat 150 na kwamba Ujenzi wa Kinyerezi 11 unaendelea
na utakapokamilika utazalisha megawati 30 zitakazoongezwa 30 kila baada ya miezi
mitatu.

Katika sekta ya ujenzi alisema Serikali imeshaanza ujenzi wa reli ya kisasa inayoanzia
Dar es Salaam hadi Morogoro, Flyovers Tazara na Ujenzi wa Bomba la Mafuta la
Hoima hadi Tanga.

Abbasi alisema uhuru wa vyombo vya habari unalindwa na Katiba kwenye kifungu cha saba cha Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari na kusisitiza hadi kuna magazeti 430, redio zaidi ya 140 na Vituo vya Runinga 32.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search