gOOD nEWS: WHC yashusha neema kwa watumishi Makao Makuu Dodoma...#share
KAMPUNI ya Watumishi Housing (WHC) imesema imeanza ujenzi wa
nyumba 159 makao makuu ya nchi Dodoma katika kuunga mkono uamuzi wa serikali
kuhamishia shughuli za kiserikali katika mkoa huo.
Hayo yamebeinishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa WHC Fred Msemwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema nia yao
ni kuboresha maendeleo ya nchi.
“Watumishi Housing tumejipanga kuwajengea watumishi nyumba
bora na za kisasa mkoani Dodoma katika eneo la Njedengwa, lililopo mkabala na
eneo la Kisasa Dodoma,” amesema Msemwa.
Amesema kutokana na mpango wa serikali wa kuhamishia shughuli
zake mkoani Dodoma kuja na fursa nyingi ikiwa moja wapo ni kuendeleza makazi ya
watumishi, WHC ni jukumu lao la msingi kuhakikisha wanapata makazi bora na ya
kisasa kwa bei nafuu.
Msemwa amebainisha kwamba kutokana na hali hiyo wameandaa
ardhi ya ekari 55 za ardhi mkoani humo ambapo wanatarajia kujenga nyumba 500.
Nyumba 159 zitajengwa katika awamu ya kwanza kwaajili ya watumishi watakao kuwa
wakihamia Dodoma na wale wanaoishi Dodoma.
Ameweka wazi bei ya nyumba ya vyumba vitatu itaanzia sh.
milioni 46 na amebainisha kuwa ujenzi wa nyumba hizo utachukua muda wa miezi
nane kukamilika ambapo amesema zitakuwa za aina mbili yani zilizoisha kabisa (full
finished) na zile zitakazokuwa zimeisha kwa asilimia 80, hivyo mtumishi atakuwa
na fursa ya kuingia na kuishi huku akimalizia kwa kadri anavyopenda.
Aidha amesema bei za nyumba zilizokamilika itakuwa sh.
milioni 59 pamoja na VAT na zile ambazo zimekamilika kwa asilimia 80 tayari kwa
kutumika zitakuwa sh.milioni 46 pamoja na VAT huku zikilipwa kwa njia ya
malipo endelevu wakati wa au wa mkopo wa bei nafuu toka kwa benki washirika na
kurejesha ndani ya mwaka mmoja hadi miaka 25.
Kwa upende mwingine Mkurugenzi huyo amesema wamepokea mssada
wa vifaa vya upimaji wa viwanja na miji ambavyo vitawasaidia katika kutoa
huduma zote za makazi kuanzia uuzaji wa viwanja vilivyopimwa pamoja na nyumba
zilizokamilika.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment