nEWS: Rwebangira aomba kufika Magogoni kumfunda JPM...#share
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi wa Taasisi ya Milemine
East Refining Salvatory Rwebangira ameomba kuonana na Rais John Magufuli
ili amwelezee ujuzi na uzoefu wa zaidi ya maiaka 25 alionao katika masuala
ya utafiti wa madini na mimea kwa ajili ya utengenezaji wa dawa za binadamu.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam
mkurugenzi huyo alisema katika kipindi chake alichofanya utafiti amegundua
masuala mengi kwenye madini yanayoweza kutumika katika viwanda na utengenezaji
dawa hizo hivyo kuonana naye itakuwa fursa nzuri ya kumuelezea njia
zitakazoisaidia nchi kuinua uchumi wa viwanda.
"Namuomba Rais Magufuli pamoja na shughulli zake
kuwa nyingi na finyu akihudumia taifa zima anipatie muda wa kumuona
nimshukuru binafsi na kwa niaba ya watanzania, pia nipate nafasi ya kutoa neno
langu la ujuzi na uzoefu kutokana na historia yangu ya utafiti,"
alisema Rwebangira.
Aidha Rwebangira amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi
zake za kuleta mabadiliko nchini kwani kwa muda mchache aliokaa madarakani
amenuunua ndege tatu kwa ajili ya kuboresha usafiri wa anga na kukuza utalii
wa nchi.
Amesisitiza kuwa amepunguza idadi ya wafanyakazi hewa
na wenye vyeti feki huku akibainisha Serikali ya Awamu ya Tano imeafanya
kazi ya kupambana na dawa za kulevya ambazo zilikuwa zikiangamiza vijana.
Pia amesema uongozi wa awamu hii umeboresha huduma ya
maji kwani hapo mwanzo lilikuwa suala kero kubwa nchi nzima hivyo
imewapunguzia wananchi adha ya kutembea umbali mrefu.
Amefafanua kuwa Serikali inayoongozwa Rais Magufuli
imeanza Ujenzi wa Reli ya Kisasa inayoanzia Dar es Salaam hadi Morogoro
jambo ambalo limewashangaza hata wazungu.
Katika hatua nyingine, amezipongeza Tume za Kuchunguza
Makinikia ikiwemo Kamati ya kwanza iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim
Mruma na ya pili iliyosimamiwa na Profesa Nehemiah Osoro.
Wakati huo huo, Rwebangira amempongeza Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa kwa kufuatilia na kusimamia kwa nguvu azma ya viwanda na
uwajibikaji wenye nia ya dhati ya kulirudisha taifa kwenye mstari uliionyooka.
Na Hussein
Ndubikile
No comments:
Post a Comment