fURSA: Watanzania watakiwa kuchangamkia fursa ujenzi bomba la mafuta ghafi...#share
JUMUIYA ya watoa Huduma wa Sekta ya
Mafuta na Gesi (ATOGS) imewataka wadau kuchangamkia fursa zilizopo kabla na
baada ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
Ujenzi huo unaotarajiwa kuanza hivi
karibuni utagharimu Dola za Marekani Biliioni 3.5 sawa na Sh. tirioni 8 za
Kitanzania na unatarajia kuzalisha ajira kati ya 10,000 hadi 30000.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar
es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa
(ATOGS) Abdulsamad Abdulrahim akizungumza na waandishi wa habari, amesema wanaunga
mkono Serikali ya Tanzania kwani watoa
huduma waliopo Nchini wameonesha uwezo na utayari wa kutoa huduma nyingi katika
mradi huo na kuchangamkia fursa zitokanazo na mradi.
Aidha ameteja fursa hizo zitokanazo na mradi
huo wanazohamasishwa watoa huduma kuchangamukia
kuwa ni pamoja na ujenzi, ununuzi, uwezeshi, huduma za bima, kibenki, fedha,
kisheria, ulinzi, chakula na dharura.
Amesema uongozi umeona umuhimu wa
kuzipokea fursa na Makampuni yanayotoa huduma yamekwishajiunga na ATOGS na
kuyaita makampuni mengine kujiunga ili yaweze kupata fursa zinazopatikana sasa
na nyingine zinazoendelea kufunguka.
“Baada ya ufungunzi rasmi wa ujenzi
wa bomba la mafuta na gesi utakaofanyika jumamosi wiki hii tarehe 5 mwezi 8
mwaka huu ambao mgeni rasmi ni Rais John Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri
Kaguta Museveni katika kufanikisha ufunguzi wa mradi huo kwa ajili ya manufaa
ya nchi mbili,”amesema Abdulirahim.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Juliana Palangyo amesema mradi unafursa kubwa na
kuwaomba watoa huduma kupitia (ATOGS) kuungana katika kupata fursa inayotokana
na mradi huo.
“Mradi huu una fusra nyingi kama
ujenzi, biashara, utoaji huduma na chakula, zote hizi ni fusra zinazoitaji watu,
pia ujenzi huu wa bomba la mafuta utaifikia mikoa 8 na wilaya zake ambayo ni
Singida, Tanga, Shinyanga, Geita, Dodoma, Manyara, Kagera na Kahama ndani ya
miezi 24,” amesema Palangyo.
Na Dalila Sharif.
No comments:
Post a Comment