gUMZO lA aSUBUHI: Mambo 34 yaliyomkuna Mbunge Maftaha wa CUF kwa JPM hata akapiga 'kura ya NDIO'.. #SHARE..

Huku hali ya 'upepo mbaya' wa kisiasa ukiendelea kukipiga Chama cha CUF, MBUNGE wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma kuptia tiketi ya chama hicho ametaja baadhi ya mambo katika 34 yaliyomfanya kupiga kura ya ‘ndiyo’ kwenye mchakato wa upitishaji Bajeti kwa mwaka 2017/18.


Baadhi mambo hayo ni pamoja na Bajeti kutetea rasilimali za madini, kuondoa kodi kwenye maeneo mengi yanayogusa wananchi na kuondoa tozo zilizokuwa zikitesa wafanyabiashara.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nachuma alisema kwa kiasi kikubwa kuoendolewa tozo kwenye mazao kutawezesha upatikanaji chakula kwa wingi na bei haitapanda.

“Mimi mbunge ninayejitambua, nampongeza Rais John Magufuli kwa kusimamia rasilimali za nchi vizuri licha ya kuwapo watu wasio na sera wanaoponda anavyofanya, hivyo namsihi akaze buti,” alisema.

Aliongeza kuwa anaunga mkono bajeti zote zilizopitishwa pamoja na mikataba ya madini iliyosainiwa na kupitishwa na Serikali ya sasa.

Aidha, alisema mambo mengine katika hayo 34 anatarajia kuyataja katika mikutano yake ya hadhara anayotarajia kuifanya jimboni hivi karibuni.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search