kENYA eLECTIONS: Marekani na Uingereza wajitosa uchunguzi wa kuuliwa Chris Msando wa IIBC #SHARE

Marekani na Uingereza wamejitolea kusaidia katika uchunguzi wa mauaji ya kutatanisha ya kaimu mkurugenzi wa masuala teknolojia wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, kabla ya kufanyijka kwa uchaguzi mkuu.

Gazeti la Daily Nation lilisema kuwa balozi wa Marekani nchi Kenya Robert Godec na wa Uingereza Nic Hailey, walilaani mauaji hayo na kuongeza kuwa wanakaribisha kujitolea kwa serikali katika kuchunguza kisa hicho.



Chris Msando alikuwa msimamizi wa mifumo ya kompiuta kwenye uchaguzi ambao utaandaliwa Jumanne, mifumo ambayo ingezuia wizi wa kura.

Mwili wa Bwana Msando ulipatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhia maiti jijini Nairobi jana Jumatatu.

Kisa hiki kinatokea ikiwa imesalia juma moja kabla ya kuandaliwa uchaguzi mkuu nchini Kenya ambao utafanyika tarehe 8 Agosti.

Polisi wanasema kuwa mwili Msando pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la Kikuyu lililo viungani mwa mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City Mortuary.

Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake - BBC

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search