kIMATAIFA: Dangote sasa kuvunja record ya ujenzi wa kiwanda kikubwa zaidi cha kuchakata mafuta Duniani.. #share

Binadamu tajiri zaidi Barani Afrika Aliko Dangote, ameombwa na serikali ya Nigeria kukamilisha ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta mapema ya muda wake rasmi wa kukamilika mwaka 2019.


Gazeti la Premium Times la nchini Nigeria lilimnukuu waziri wa mafuta Ibe Kachikwu akisema, "Rais Buhari angependa kupata kuwa anakuja kukifungua kiwanda kikubwa kama hiki kabla ya muhula wake kukamilika"

"Ninaona tarehe ya kukamilika ujenzi wa kiwanda hiki ni Disemba mwaka 2019, lakini ninajua unaweza kuelewa kuwa ningependa mradi huu kukamilika mapema kuliko ulivyopangwa," waziri alinukuliwa akimuambia Dangote alipotembelea mradi huo mjini Lagos.

Kiwanda hicho ndicho kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta duniani kilichojengwa eneo moja na cha pili kwa kutengeneza mbolea duniani.
Licha ya kuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa zaidi wa mafuta duniani, Nigeria hununua asilimia kubwa ya mafuta kutoka nje na kwa sasa inakabiliwa na uhaba mkubwa.

Wakati ujenzi wa kiwanda hicho utakamilika kitakuwa na uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 kwa siku kwenda petroli, gesi ,mafuta ya taa na ya ndege.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search