nEWS: Baada ya 'pedi mashuleni nchini Kenya' Rihanna nae apeleka baiskeli kwa wanafunzi Malawi.. #share.

Ikiwa ni mojawapo ya juhudi za Dunia kumkomboa mtoto wa kike kielimu,.. SuperStar katika tasnia ya muziki na urembo nchini Marekani, Mwanandada Rihanna, kupitia mojawapo ya ushirikiano kati ya wakfu wa Rihanna & Clara Lionel Fountaion kupitia kampuni Ofo kutoka China, imeanza kutoa ufadhili wa baiskeli kwa watoto wa kike Nchini Malawi.


Rihanna aki-show-off pamoja na mwanawe na mpenzi wake.. 
Kampeni hiyo maarufu kwa jina 1km Action, itatoa ufadhili huo ili kuwasaidia mamia ya wasichana kuhudhuria shule za upili nchini malawi.

Wale watakaofuzu kupata ufadhili huo watapewa baiskeli ili kuhakikisha wanakwenda shule na kukamilisha masomo yao ya upili ambapo kwa sasa inakisiwa ni chini asilimia 10 ya wanafunzi hukamilisha masomo yao Nchini humo.. sababu ya usafiri ikitajwa miongoni mwa vikwazo vikuu.

''Nina furaha sana kuhusu ushirikiano na wakfu wa Clara na Ofo kwa sababu utawasaidia wasichana wengi dunini kupata elimu bora, pia watamaliza shule wakiwa salama zaidi kwani itawapunguzia mwendo kutoka majumbani mwao hadi mashuleni'' alisema Rihanna akielezea furaha yake juu ya mradi huo..

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search