wORLD nEWS: pICHA 4 za Jengo la Torch 'Marina' Tower likiwa katika janga jengine la moto..#share

Dunia ikiwa bado ndani ya kumbukumbu nzito ya janga la moto la Grenfell iliuyokea jijini London na kuzua taharuki kwa wajenzi, moto mwengine mkubwa umezuka na kuliteketeza jengo maarufu kwa watalii Jijini Dubai, na miongoni mwa majengo marefu zaidi Duniani la Torch Tower, ikiwa ni tukio la pili kwa jengo hilo ndani ya miaka miwili, baada ya ile nyengine mbaya zaidi ya mwaka 2015.

Picha za awali za Torch Marina Tower enzi za ubora wake kabla ya mkasa wa jana wa moto
Picha zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zilionyesha moto huo ukisambaa hadi katika jumba hilo huku vifusi vizito vya maeneo yaliyoteketezwa vikionekana vikiporomoka..


Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za mamlaka ya mji huo, wafanyakazi na watoa huduma za zima moto walifanikiwa kuwaondoa watu na wakafanikiwa kuudhibiti moto huo ambao hadi sasa chanzo chake hakijajulikana.. 

Bado juhudi za kutambua uwepo wa majeruhi na vifo unaendelea na mamlaka imefungua account maalum katika mtandao wa twitter kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi wa mkasa huo.

Matukio360 ipo kuendelea kukupa taarifa, endelea kufuatana nasi kupitia uzi huu..






About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search