nEWS:JPM aipoka JKT ardhi na kurudisha mikononi mwa wananchi Tanga...#share
RAIS Magufuli
amerudisha kwa wananchi eneo la ardhi ambalo Jeshi la Kujenga Taifa (Mgambo JKT)
Mkata, Wilayani Handeni Mkoani Tanga, lilishindwa kuliendeleza kwa muda wa
miaka saba.
Amekifia
hatua hiyo leo wakati akisalimiana na wananchi wa eneo hilo akiwa safarini, baada
ya kiongozi wa JKT kukiri kuwa walishindwa kuliendeleza katika kipindi hicho
tangu walipopewa na kijiji ili kujenga kiwanda.
Badala yake Rais
Magufuli ameagiza kiwanda hicho kijengwe ndani ya eneo la JKT ambalo tayari
lina miundombinu ya maji na umeme.
“Eneo la
mgambo JKT niameambiwa haliendelezwa katika kipindi cha miaka saba, warudishiwe
wananchi waliendeleze kwa kazi za kilimo, kiwanda mkajenge hapohapo, ardhi ya
wananchi muirudishe,”alisisitiza.
Aidha, Rais
Magufuli amewaonya vijana akiwataka kuacha kutumika kwa kutegemea fedha za
bure, badala yake wafanye kazi zikiwemo za kilimo ili kujipatia maendeleo.
Kuhusu suala
la afya, Rais Magufuli amesema Serikali imetenga Sh. milioni 800 kwa ajili ya
ujenzi wa hospitali ya wilaya huku akiwataka wananchi kushirikiana na tume
itakayoundwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Njia Wazee na Watoto kuchunguza
ubadhilifu wa sh. milioni 500 zilizotolewa awali kwa ajili hiyo.
Magufuli amesema
lazima hospitali ya wilaya ijengwe kwa kuwa hawezi kukubali eneo la kutoka
Mkata hadi Chalinze kutokuwa na hospitali ya wilaya, kwani kuwepo kwake watu wanufaika
hawatakuwa wananchi wa eneo hilo tu.
Kuhusu maji,
Rais amesema mradi kutoka Mto Wami unaotarajiwa kugharimu sh. trilioni 4, hadi
sasa serikali imeshatoa nusu ya kiasi hicho na tayari mabomba yameshatandazwa
ilikuondoa changamoto ya kukosa nishati hiyo kwa wananchi Mkata.
Aidha, amewashukuru
wananchi wa eneo hilo kwa kumpa kura huku akiahidi kuwahudumia kwa kuhakikisha
anaondoa kero zao.
Rais
Magufuli yupo safarini ambapo Agosti 5 atakutana na Rais wa Uganda, Yoweri
Museveni kwa ajili ya kuweka jiwi la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha
mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment