sPORTS nEWS: CUF yatokwa povu Zanzibar kuvuliwa uanachama CAF, yataka hatua zichukuliwe....#share
CHAMA cha Wnanchi CUF kimelaani na kupinga vikali hatua ya
Chama cha Mpira Barani Afrika (CAF) kuwavua uanachama kwani kitendo hicho
wamekifananisha na Zanzibar kuvuliwa nguo.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu
wa chama hicho Nassoro Ahmed Mazrui akizungumza na waandishi wa habari, alisema
si kitendo cha kuvumilika hata kidogo.
“Mbali ya kukilaani, bali pia ni haki yetu kukipinga. Na
zaidi ya kukilaani na kukipinga, CUF inaona tuna wajibu wa kudai kupata maelezo
ya kutosha, kutoa taarifa/taaluma ya kutosha kwa CAF na kukikatia rufani kadiri
ya Kanuni zinazohusika zilivyo ili tukisemee, tukisimamie na tukitafutie suluhu,”
amesema Mazrui.
Aidha amebainisha kwamba walitegemea viongozi wa Zanzibar na Muungano
wangelilisemea jambo hilo kwa nguvu inayopaswa kusemewa, lakini hawajaona hatua
thabiti za kuukabili msiba huo kwa Zanzibar.
Mazrui alieleza wameshindwa kusikia sauti ya kuunguruma kuzungumzia
tukio hilo, ambalo limewarudisha nyuma baada ya kuonekana wamepiga hatua moja
kubwa na ya maana kwa nchi yeo.
Amesema kuwa pamoja na kuvuliwa huko kuwa ni kwa mujibu
washeria lakini wanaona kwamba waanayo nafasi ya kuielezea CAF kuwa haiko
sahihi katika uamuzi wake kwa hoja ambazo imezitoa.
Ameeleza, CAF ilichokifanyia maamuzi ni kukosekana kipengele
cha kuchukua hatua ndani ya mipaka ya sheria kwa kesi kama ya Zanzibar ambayo
haifanani na nyengine yoyote hapa Afrika kwa waliokubaliwa wanachama wa CAF.
Amefafanua kwamba CAF imetoa hoja kuu mbili zilizopelekea
kuinyang’anya Zanzibar kiti chake katika chombo hicho. Moja, ni kwamba haiwezi
kutoa nafasi mbili kwa nchi moja kuwakilishwa na pili, ni kuwa kigezo cha
uanachama ni kuwa nchi hiyo ni mwanachama wa UN. Hoja ambazo zote wamedai
kwamba dhaifu.
Mazrui amesema CUF inaamini kuwa ni vyema hili likasimamiwa kwa makini zaidi
katika kuelekea kukata rufaa au kupinga uamuzi wa CAF wa kuitoa Zanzibar baada
ya kupitishwa na Mkutano Mkuu na tuna hoja zifuatazo:
Amesema kutokana na hali hiyo wametaka baadhi ya haya
yafanyike, wamewataka wahusika kutoka Zanzibar wasilifanyie ajizi jambo hilo na
lifuatiliwe kwa utaalamu na umakini.
Aidha ametaka wahusika waiarifu CAF kuwa kuwaambia wawakilishwe na
TFF katika mazingira yaliopo sasa ni kunakaribisha ukoloni mamboleo, kwa sababu
kikatiba na kisheria ni suala ambalo haliwezekani.
Amesema njia peke ya kutoka katika hilo ni kuishawishi CAF
iunde Tume Maalum kulifuatilia suala hili kwa kina na undani unaostahiki.
Ameeleza iwapo jambo hilo ni kwa maslahi ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, CUF imetaka kuona unakuwepo mkazo wa hali ya juu wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuhusishwa kikamilifu Wizara ya Mambo ya Nje
ambayo inapaswa kusimamia maslahi ya Tanganyika na Zanzibar kwa usawa.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment