sPORTS nEWS: FC Barcelona yabariki Safari ya Neymar kwenda PSG

Kwa muda mrefu kumekuwa na headlines zilizodaiwa kuwa ni mvutano kuhusiana na staa wa soka wa Kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona ya Hispania,Neymar kudaiwa kushinikiza kuihama Klabu hiyo na kujiunga na Paris Saint Germain ya Ufaransa.
Leo August 2, 2017 FC Barcelona wamethibitisha kumpa ruhusa Neymar kutofanya mazoezi na timu ili kuelekea kukamilisha usajili wake wa kujiunga na PSG ingawa taarifa ya Barcelona haijaweka wazi sababu za moja kwa moja za ruhusa hiyo.
Baada ya ruhusa hiyo vyombo vingi vya habari Ulaya vinaripoti kuwa Neymar anaelekea kuanza safari yake ya maisha mapya PSG ambao wameripotiwa kutenga pound Milioni 199 kwa ajili ya kuvunja mkataba wa staa huyo wa zamani wa Santos kiasi kilichopo katika mkataba wake.
“Neymar hajafanya mazoezi na timu siku ya Jumatano kwa ruhusa ya Kocha”
Kama uhamisho huo ukikamilika Neymar ndio atakuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kuuzwa katika historia ya soka. Kwa kiasi cha pound milioni 199 anachouzwa Neymar ni zaidi ya Tsh Bilioni 580 kiasi ambacho hajawahi kuuzwa wala kununuliwa mchezaji yeyote katika historia

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search