sPORTS: Dakika za 2 Haji Manara kwa Nyota Mwanjale, Nahodha Mpya wa Simba SC

Mkuu wa idara ya habari wa klabu ya Simba,Haji Manara amesema kuwa maamuzi ya Kocha Mkuu wa Simba SC, Joseph Omog kumvua unahodha mchezaji, Jonas Mkude yapo sahihi.
Mkuu wa idara ya habari wa klabu ya Simba, Haji Manara
“Mwanjale ameshakuwa nahodha wa timu ya taifa ya Zimbabwe ameshakuwa nahodha wa Power dynamo ambayo imecheza nusu fainali ya klabu bingwa Afrika, lakini ni mchezaji anayekubalika sana ndani ya timu yenyewe na anauzoefu mkubwa”.Amesema Haji Manara ambaye ni mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba SC alipoongea na mtandao maarufu wa mambo ya burudani wa Bongo5.
Manara ameongeza kuwa “Bocco hivyo hivyo ameshawahi kuwa nahodha wa Azam FC na walikuwa pamoja na kocha Omog hivyo anamjua vizuri na anaona muunganiko huu utakuwa na manufaa, unahodha sio tu kuvaa kitambaa lakini katika vyumba vya kubadilishia nguo huwa ana nafasi kubwa sana ambayo watu wengi wamekuwa hawaelewi”.
“Simba si mara ya kwanza kubadilisha nahodha kabla ya Mkude alikuwa Cholo na alivyo kabidhiwa yeye kitambaa cha unahodha hapakuwa na tatizo lolote na timu inaendelea vizuri tu”.
By Hamza Fumo 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search