Bad News: Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akionyeshwa Nguo za Lissu zilizotapakaa damu..#share

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi nyumbani kwake na kwamba hali yake ni mbaya.

Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema kwa sasa amepelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi wanakataa wakisema hawamwamini mtu yeyote.

Asubuhi, Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo wa Naibu Spika akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya kujadiliwa na Bunge kwanza.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search