NEC yateu Mbunge mwingine CUF kujaza ya aliyefariki....Pia yateua madiwani 3 viti maalumu..#share

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua Rehema Migira kuwa Mbunge wa viti maalum kupitia Chama Cha (CUF) kujaza nafasi ya Mbunge mteule Hindu Mwenda aliyefariki Septemba 1 mwaka huu.


Akizungumza jijini Dar es Salam leo Mkurugenzi Mkuu wa NEC Kailima Ramadhan, amesema wamefanya uteuzi huo baada ya kupata taarifa kutoka wa spika wa bunge, Job Ndugai kuwepo kwa nafasi moja ya ubunge kufutia kifo cha mbunge huyo mteule aliyefariki kabla ya kuapishwa.

"NEC imemteua ndugu Rehema Juma Migira kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata taarifa kutoka wa spika ambaye alitutaarifu kuwepo kwa nafasi moja ya wazi ya viti maalumu kupitia chama cha CUF baada ya aliyeteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum CUF kufariki dunia" amesema Ramadhan.

Aidha ameendelea kusema kuwa tume hiyo imefanya uteuzi pia wa madiwani wa viti maalum watatu kujaza nafasi zilizo wazi katika halimashauri za Tanzania Bara.

Ramadhan ametaja madiwani hao kuwa ni pamoja na  Jane Chungwa ambaye anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Itigi Singida,  Osana Mwinyi anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Bahi Dodoma wote Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mwingine ni Pili Mfaume kutoka Chama cha Wananchi CUF anayekuwa  Diwani wa Viti Maalum Halmshauri ya Temeke, uteuzi huo wa madiwani umefanyika baada ya tume kupata taarifa ya kuwepo kwa nafasi hizo wazi kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa.

Na Abraham Ntambara

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search