KAMATI ya Uchunguzi upotevu wa Madini ya Almasi Yawakaanga wajumbe wa bodi na wote waliohusika kusimamia Mgodi...Pia wamo Mawaziri Wamagufuli....#share
KAMATI ya Bunge iliyoundwa kuchunguza upotevu wa
madini ya Almasi, imependekeza wajumbe wote wa bodi na watu waliohusika na
kusimamia mgodi wa madini hayo, wahojiwe na ikibainika wamehusika wachukuliwe
hatua.
Akisoma ripoti ya kamati hiyo ambayo ilikabidhiwa
kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye naye alimkabidhi Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mussa Azan Zungu amesema wamebaini madudu
mengi.

Madudu hayo ni pamoja na upotevu wa kodi, kutosimamiwa vyema kwa uchimbaji wa madini hayo, tofauti kubwa kati ya takwimu zinazotolewa na taasisi za Serikali juu ya kiasi kilichopatikana na kuuzwa cha madini hayo na udanganyifu kuhusu hali na gharama za mitambo.
“Kamati inapendekeza Serikali iwahoji wajumbe wa
bodi ya migodi hii na wote wanaohusika na ikibainika kuwa walihusika katika
mapungufu waliyoyaona wachukuliwe hatua,” alisema Zungu.
Watendaji hao wa Serikali pamoja na wajumbe wa bodi
za madini ni, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini katika Serikali za Awamu za
Nne na Tano, Profesa Sospeter Muhongo.
Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi),
George Simbachawene, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini katika Serikali ya
Awamu ya Nne, William Ngeleja, na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa
Serikali ya Awamu ya Tatu, Maokola Majogo.
Watendaji wengine ni aliyekuwa Katibu Muu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, Profesa Abdulkarim Hamis Mruma na Profesa
Isaya Jairo.
Akizungumza kuhusu takwimu hizo, Zungu alisema
takwimu zilizokuwepo kwa Wakala wa Madini Tanzania (TIMA) zinaonesha kuwa
kuanzia mwaka 2007 hadi 2017, kiasi cha karati milioni 1.5 zilizalishwa na
kuuzwa kwa dola za Marekani milioni 374.5 sawa na sh bilioni 823.9.
Kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini, takwimu
zilizokuwepo zilionesha kuwa ni karati milioni 1.4 ndizo zilizozaliswa na
kuuzwa kwa dola za Marekani milioni 362 ambazo ni sawa na sh bilioni 796.4 huku
tofauti ikiwa ni sh milioni 27.5.
Na Mwandishi Wetu




No comments:
Post a Comment