Habari Njema: Benki ya kilimo yaongeza kiasi cha mikopo kutoka Sh bilioni 1 hadi sh bilioni 8.917
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)imesema imeongeza kiasi cha mikopo kwa
wakulima wadogo wadogo kutoka Sh bilioni 1.0 hadi Sh bilioni 8.917 huku ikibainisha
kukopesha wakulima 2,610 lengo likiwa kuwanufaisha na kuwakawamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TADB,Francis Assenga wakati akizungumza na wanahabari kuhusu benki hiyo kutimiza
miaka miwili ya utoaji huduma na mikakati yake ya kujitanua kupitia kongani.
Amebainisha kuwa tangu benki hiyo ianzishwe imekuwa ikipiga hatua katika
kuwahudumia wakulima ikiwemo kuwawezesha kupata mikopo inayowasaidia kufanya kilimo
cha kisasa na chenye tija huku akisisitiza benki hiyo imejzatiti kuwafikia wakulima wote
''Benki inaendelea kufanya uchambuzi wa miradi 17 yenye thamani ya zaid8i ya sh
bilioni 35.473 pia tumeweza kukopesha kutoka vikundi nane hadi vikundi 21, taasisi
moja ya umma na kampuni moja ya maziwa,'' alisema Assenga.
Ameongeza kuwa TADB imeweza kuvijengea uwezo vikundi 672 vya wakuluima wadogo
wadogo vyenye jumla ya wanachama 91,684 kutoka vikundi 336 vilivyokuwa vinajumuisha
wakulima ha9o 44,000 katika mikoa ya Iringa, Morogoro na Tanga.
Amefafanua kuwa benki hiyo imewaunganisha wakulima wadogo 2,328 na wanunuzi kwenye
mnyororo wa thamani wa mazao ya mahindi,mpunga, mbogamboga na miwa.
Aidha, amesema TADB imeweza kupata fedha zaidi za kukopesha kutoka Serikalini kiasi
cha Sh bilioni 209.5 huku akibainisha nusu ya fedha hizo zimeshapatikana kutoka
Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Pia amesema wataongeza wigo wa utoaji huduma kutoka mikoa sita kwenda kanda nane
kwa uratibu wa kongani ya idadi ya kipaumbele toka mikoa 14 hadi 20 kulingana na
vipaumbele vya mikoa.




No comments:
Post a Comment