Wizara ya Afya yapokea sh.bilioni 227.76 kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya nchini... #share
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto imepokea shilingi Bilioni 227.76 kutoka kwenye mfuko wa pamoja (Health Basket Fund) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya afya nchini.
Akizungumza wakati wa kupokea fedha hizo leo jijini Dar es Salaam , Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika uboreshaji wa huduma za afya nchini.
“Fedha hizi zitasaidia pia kutoa huduma za chanjo kwani ni afua muhimu kwa wananchi hususan katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchini”
Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kwa mara ya kwanza wameamua kupeleka fedha hizo moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuepuka changamoto za vituo hivyo kukosa dawa muhimu mara kwa mara.
Mbali na hayo amesema kuwa asilimia 90 ya fedha hizo zinaenda moja kwa moja kwenye vituo vinavyotolea huduma za afya ngazi ya Halmashauri na asilimia 10 itatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za usimamizi wa kisera katika sekta ya afya.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema fedha hizo pia zitasaidia katika kuimarisha miundombinu katika vituo vya afya na zahanati ili viweze kutoa huduma za upasuaji wa dharura kwa ajili ya akina mama wajawazito wanaokabiliwa na uzazi pingamizi .
“Tunapopeleka fedha hizi moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya hivyo tunahitaji mtu mwenye weledi na ujuzi ambaye ataangalia namna fedha zinavyotumika bila kuvunja sheria,kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za Serikali hivyo tutahakikisha adhima hii inafikiwa kwa kutatua tatizo la watumishi wa sekta ya afya nchini.
Pamoja na hayo,Katibu mkuu huyo amekubali ombi la Balozi wa Dernmak kuleta fedha kwa ajili ya matumizi ya wakimbizi wanaoingia nchini,hivyo Wizara yake itakaa na kuandika andiko la makubaliano ya Serikali litakalosaidia kujua fedha hizo zitakuja kwa matumizi gani.
Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar Jensen kwa niaba ya wadau wa mfuko huo amesema kuwa mbali na Fedha hizo kushughulikia maswala ya afya hapa nchini pia zitakuwa na shughuli mbalimbali za maendeleo .
“Mbali na kushughulikia masuala ya afya pia napendekeza fedha hizi zihusike katika kuhudumia wakimbizi wanaongia Tanzania hasa katika maeneo ya Kigoma na Kibondo” alisema Bw. Jensen.
Na Mwandishi Wetu

No comments:
Post a Comment