Hashim Rungwe apeleka kilio kwa Msajili wa Vyama kwa kudhoofisha utendaji wa vyama vya upinzani.. #share
UONGOZI wa Chama cha Ukombozi wa Umma (chaumma) imedhamiria kukuandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kwa madai kuwa ameshindwa kusimamia wajibu wake katika kuisimamia Sheria namba tano ya mwaka 1992 ya usajili wa vyama vingi vya siasa.
Dhamira hiyo imetolewa katika kikao cha Kamati Kuu Taifa ya Chauma kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam kikiwa na lengo kutathimini mwenendo wa taifa.
Akizungumza baada ya kikao hicho Mwenyekiti wa Chama hicho Hadhi Tunywe amesema Sheria namba tano ya vyama vya siasa imekuwa ikiminywa na kuchangia vyama hivyo kushindwa kufanya shughuli zao za kisiasa ipasavyo.
"Tunatarajia kukuandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kushindwa kuisimamia Sheria hii ipasavyo, vyama vya siasa havifanyi kazi zake kwa kuminywa kwa sharia hiyo," amesema Tunywe.
Naye Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Zanzibar Mohamed Masoud amesema kupitia kikao hicho wamedhamiria kuomba kujua tafsiri ya sheria hiyo ambayo inawaruhusu wanasiasa kutangaza vyama vyao katika kila ya nchi.
Kwa upande wake Alli Juma amesema kushindwa kusimamiwa kwa sheria hiyo kumpoteza maana na uhalali wa vyama vya siasa kitokana na kushindwa kufanya mikutano wakati mikutano na shughuli za kisiasa ni haki ya kila chama na wanasiasa kwani inatambulika katika Katiba ya nchi.
Aidha Chama kumlaani kitendo cha kupigwa risasi kwa Rais wa Chama cha Mawakili Yanafanyika (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema) kilichofanywa na watu wasio julikana.
Kutokana na tukio hilo chama hicho kimetoa pole kwa Spika wa Bunge Job Ngugai, familia ya Lissu, wabunge na Chama cha chakula na watanzania wote.




No comments:
Post a Comment