sPORTS nEWS: Sanga,Yahya kuwania kiti Bodi ya Ligi.....#share


KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha majina ya wagombea wafuatao kuwania uongozi katika  nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Kamati ya Uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ambapo Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga atachuana na Ahmad Yahya atayetetea nafasi ya uenyekiti. 


                                        Clement Sanga
Sanga na Yahya wanatokea katika klabu za Ligi Kuu ya Tanzania, za Yanga ambapo Sanga anakaimu nafasi ya uenyekiti baada ya Yusuf Manji kujiuzulu kwa sabau za kiafya.

Kwa wa mujibu wa taarifa ya  TFF iliotolewa kwa vyombo vya habari leo, majina hayo yamepitishwa mara baada ya kuwafanyia usaili Jumapili Septemba 3, mwaka huu kwenye Ukumbi wa TFF, Dar es Salaam. Uchaguzi utafanyika Oktoba 15, mwaka huu. 

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi inayotokana na kanuni za uchaguzi za TFF, majina hayo yanapaswa kutangazwa sasa.

Ahmad Yahya (kushoto) kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura
                       
Wanaowania nafasi ya ujumbe ni Hamisi Madaki na Ramadhani Mahano wanatokea Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Pia yumo Almasi Kasongo anayewania nafasi hiyo  kupitia Klabu za Ligi Daraja la Kwanza huku Edgar Chibura akiwania nafasi ya ujumbe kupitia Klabu za Ligi Daraja la Pili wakati huo huo,

Wakati huohuo, TFF, imeagiza Makatibu wa Vyama vya Mikoa kutuma haraka majina ya timu mabingwa wa mikoa wa soka la wanawake wa msimu wa 2016/17.

 Viongozi wa mikoa wamekumbushwa kutuma timu ili kufanya maandilizi ya haraka ya Ligi Ndogo itakayofanyika Septemba 22 hadi 29, mwaka huu.

Ligi Hiyo ndogo inachezwa kutafuta timu mbili zitakazopanda daraja kucheza Ligi Kuu soka ya wanawake msimu wa 2017/2018.

 Huu ni msimu wa pili wa ligi ya wanawake kwani msimu uliopita, timu shiriki zilikuwa 12 na Mlandizi Queens ya Pwani iliibuka bingwa wa kwanza katika historia ya soka hapa nchini.


Mara baada ya kumalizika kwa Ligi Ndogo, TFF itaanza taratibu za kupanga kuanza kwa Ligi Kuu kwani wakati huo tayari tutafahamu timu ambazo zimepanda. Ligi Ndogo haitahusisha timu ambazo zimecheza Ligi Kuu msimu wa 2016/17.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search