Mawakili wazidi Kuandamwa na watu Wasiojulikana...Baada ya Ofisi za IMMMA Advocatse kulipuliwa...Ofisi ya Wakili wa Manji yavamiwa, kabati la Nyaraka muhimu lakwapuliwa...#share

WATU wasiojulikana wamevamia ofisi ya Wakili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusufuali Manji, Hudson Ndusyepo na kuiba kabati maalumu la kuhifadhia nyaraka muhimu na fedha, ambapo waliiba Sh milioni 3.7.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam Ndusyepo, amesema watu hao walifanya tukio hilo saa tisa usiku, ambapo walipanda hadi gorofa ya tatu wakaingia ofisi kwao na kuchukua kabati hilo.

Amebainisha kwamba kabati hilo lilikuwa na Sh milioni 3.7, leseni, hati za nyumba za wateja na nyaraka mbalimbali ambazo ni muhimu katika ofisi yao.

Hata hivyo amesema nyaraka hizo si zao peke yao kwani kuna nyaraka pia za watu wengine kwa kuwa  wao ni Kampuni ya Prime Attorneys.

Ndusyepo amesema ofisi zao zipo Upanga, Dar es Saalam  barabara ya Umoja wa Mataifa (UN), mtaa wa Kalanga, ambapo tukio hilo wakati linatokea walikuwa nyumbani kwao na jengo hilo linawalinzi ambao wanahakikisha sehemu hiyo inakuwa salama.

 “Kwa jinsi kabati hilo lilivyo ni lazima libebwe na watu zaidi ya sita, kwa sababu ni imara hata moto ukiwasha jengo kabati hilo haliwezi kuunguz, sasa nashangaa hawa watu badala ya kuvunja na kuiba wao wakalichukua lote,”alisema Ndusyepo

Wakili huyo amesema watu hao hawakuiba kitu kingine zaidi ya hilo kabati, kulikuwa na simu, kompyuta na kompyuta mpakato ‘Laptop’, lakini wao hawakuangaika na vitu hivyo.

Amesema wamesharipoti kituo cha polisi, kwa hiyo polisi wanaendelea na uchunguzi wao, wataendelea kutoa taarifa pindi tu, watakapopewa na askari kwa sababu kazi kubwa wanaifanya wao.

“Tangu asubuhi hadi jioni hii sijala chochote nahangaika na suala hili, yaani kwenye kabati hilo kulikuwa na nyaraka muhimu sana, ngoja tusubiri taarifa ya polisi, mwisho wetu ni kutoa taarifa na kuwaachia wao,” alisema 

Hata hivyo, alisema wamesikitishwa na tukio hilo kwa sababu hivi sasa itabidi kazi nyingi zisimame kutokana na nyaraka ambazo zimeibiwa na watu hao, jambo ambalo linawarudisha nyuma kiutendaji.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search