Sports News: Mahakamani Kisutu leo Malinzi na wenzake kesi yao imeahirishwa...Warudishwa rumande hadi ...#share


ALIYEKUWA Rais Wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchin (TFF) Jamal Malinzi na wenzake wawili, leo wamefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi yao inayowakabili.

Malinzi na wenzake wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao pamoja na kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

Aidha kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 21 mwaka huu baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo kutokuwepo kutokana na kuwa na dharura.

Hayo yamebainishwa na Wakili wa Serikali, Faraj Ngokah mbele ya mahakama na kusema upelelezi wa kesi hiyo hujakamalika huku ikielezwa kuwa Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Wilbard Mashauri amepatwa na dharura.

Kutokana na hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 21 mwaka huu itakapotajwa kwa mara nyingine.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search