sPORTS nEWS: TFF yaweka Sheria za Soka Pembeni...Busara yatumika kumtoa Buswita wa Yanga Kifungoni...#share

SAKATA la kiungo mshambuliaji Pius Buswita kufungiwa, limefika mwisho baada ya kupatiwa ufumbuzi na mchezajii huyo atakuwa na nafasi ya kuichezea Yanga katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.


Sakata hilo lilitokana na mchezaji huyo  kusaini mikataba miwili tofauti ya kuzitumikia klabu za Simba na Yanga jambo ambalo lilisababisha kufungiwa mwaka mmoja na kamati ya katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kwa kuwa ni kinyume na sheria mchezaji mmoja kusaini sehemu mbili tofauti.

Akizungumzia suala hilo leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, Elias Mwanjala amesema klabu hizo mbili zimefanya mazungumzo nakuafikiana juu ya mchezji huyo.

Mwanjala amesema kuwa baada ya Simba na Yanga kukubaliana juu ya mchezaji huyo ili atoke kifungoni, Yanga itatakiwa kuilipa Simba shilingi milioni 10 ambazo Buswita alizichukua aliposaini Simba.

Amebainishwa kuwa Buswita atakuwa tayari kuitumikia klabu yake Mpya ya Yanga itakapokuwa imekamilisha kuilipa Simba kiasi hicho cha Fedha.

Na Mwandishi Wetu


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search