Polisi na Wanajeshi 53 wauawa..Soma habari kamili na Matukio360..#share
MAOFISA Usalama nchini Misri wamesema, idadi ya wanajeshi na polisi waliouawa katika mapambano na wapiganaji wa Kiislamu katika eneo la Bahariya Magharibi mwa Jangwa imefikia 53.
Wizara ya Mambo ya Ndani nchini humo, imebainisha vikosi hivyo vya usalama wakati vikiwasaka wapiganaji wa Kiislamu waliviziwa katika chemchem ya maji ya Bahariya umbali wa kilomita 200 kusini mashariki mwa Cairo na kushambuliwa.
Pia, imesema wapiganaji wa Kiislamu 15 wameuawa katika makabiliano hayo.
Vyanzo vilivyo karibu na maofisa usalama vinasema msafara huo ulishambuliwa kwa roketi na wapiganaji hao pia walitumia vilipuzi. Duru za usalama zinasema kuwa wapiganaji walikuwa na uelewa zaidi wa eneo hilo na ofisa wa jeshi aliyetoa amri ya kuvamia alishindwa kuagiza wanajeshi kuimarisha kikosi chake.
Hata hivyo hakuna kikundi chochote kilichodai kuhusika ingawa kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa juu ya wapiganaji wa kikundi kinachofahamika kama Hasm, kilichowahi kushambulia majeshi ya usalamasiku za nyuma. Hata hivyo, Twitter ya kikundi hicho inayotumiwa mara kwa mara kutoa taarifa haijafanya kazi tangu Oktoba 2.
Tangu jeshi lilipomwondoa madarakani Rais Mohamed Morsi wa Muslim Brotherhood, makundi ya kigaidi yameongeza sana mashambulizi yao dhidi ya wanajeshi na polisi.
Brotherhood, waliowahi kuwa kundi kubwa la upinzani nchini wamekanusha kuhusu katika machafuko.
Mohamed Morsi alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012, lakini jeshi lilimpindua mwaka mmoja baadaye baada ya kuibuka maandamano ya kupinga sheria ya Kiislamu zinaosababisha mgawanyiko.
No comments:
Post a Comment