Mshtakiwa Rugemalila aibua mapya mahakamani....soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abdulrahim Sadiki, Dar es
Salaam
MFANYABIASHARA James
Rugemalila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha ameieleza Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anahitaji kuonana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP)
ili ampe ushahidi wa nani anayepaswa kukamatwa katika kesi hiyo.
James Rugemalila wa pili kutoka kushoto akiwa mahakamani
Disemba 8,2017 Rugemarila
aliieleza mahakama hiyo kuwa anahitajika ushirikiano baina yake na upande wa mashtaka
ili kumbaini mwizi wa bilioni 309 za Serikali.
Mbali ya Rugemarila,
Mshtakiwa mwingine ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ambapo kwa pamoja
wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababishia
Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na bilioni 309.
Rugemarila aliyaeleza hayo
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa
Takukuru, Leornad Swai kudai upelelezi
wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo,
Rugemarila alinyoosha mkono ambapo amesema kuwa anaushukuru upande wa mashtaka
ulimchukua gerezani na kumpeleka Upanga kwa mahojiano na kumrudisha salama
gerezani.
"Leo nimekuja na
ushahidi, hivyo naomba nikutane na DPP ili niweze kumsaidia kumjua mwizi
anayepaswa kukamatwa, kwani lengo letu ni kuonyesha kuwa tupo
Innocent,".alieleza Rugemarila.
Kutokana na maelezo hayo,
Hakimu Shaidi alimtaka Rugemarila kuwasiliana na mawakili wake ili waandike
barua ya kuwasilisha kwa DPP kuhusu suala hilo la ushahidi wake, ambapo
ameahirisha kesi hiyo hadi January 5,2018.




No comments:
Post a Comment