Wajumbe 613 UVCCM kushiriki mkutano mkuu...soma habari kamili na matukio360..#share


Alex Stephen, Dodoma

Jumla ya wajumbe 613 watashiriki mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)  unaotarajia kuanza kesho mjini Dodoma.
Kaimu Katibu wa UVCCM, Shaka Hamidu Shaka

Kaimu Katibu wa UVCCM Shaka Hamidu Shaka amesema kuwa maandalizi yote kuhusu Mkutano huo yamekamilika.

Shaka amesema mkutano huo utafunguliwa na Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli na utafanyika katika chuo cha mipango cha mjini Dodoma.

Akizungumzia nafasi zinazogombewa amesema ni nafasi ya Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti, wajumbe watano wa Halmashauri Kuu kundi la vijana na wajumbe wawakilishi kwenye jumuiya.

Katibu huyo amesema jumuiya hiyo imejipanga kikamilifu kuona mkutano huo wa 9 ukifanyika kwa amani na utulivu na akaonya wagombea kufanya kampeni za mwisho kwa ustaarabu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search