Aliyekamatwa na mamilioni uwanja wa ndege apandishwa kizimbani...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abdulrahim Sadiki, Dar es
salaam
Siku chache baada ya Rais
John Magufuli kubainisha kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha fedha katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere
(JNIA) aliyekamatwa na fedha hizo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
Mshtakiwa huyo ni raia wa
Uganda, ambaye ni Kalani wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA, Winfred Businge (33).
Busige amefikishwa
mahakamani akikabiliwa na kosa la kushindwa kuelezea kwa mamlaka ya forodha
fedha alizokamatwa nazo Airpot ambazo ni USD Milioni moja takribani bilioni mbili.
Wakili wa serikali
mwandamizi, Awamu Mbagwa amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa
mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja.
Amedai kuwa kosa hilo
amelitenda kinyume na kanuni za sheria za utakatishaji fedha, ambayo haimnyimi
mshtakiwa dhamana.
Wakili Mbagwa amedai kuwa
Businge ametenda kosa hilo Disemba 11,2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA).
Inadaiwa akiwa ndani ya jiji
la Dar es Salaam alikutwa ameingia nchini akiwa na USD Milioni 1 (zaidi ya
Sh.Bil 2)ambazo alishindwa kuzitolea maelezo kwa wakala wa forodha.
Baada ya kusomewa kosa hilo,
mshtakiwa alikana kosa, ambapo wakili Mbagwa alieleza kuwa upelelezi wa kesi
hiyo umekamilika na anaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya
awali.
Hata hivyo, wakili wa
utetezi Emmanuel Safari alimuombea dhamana mteja wake.
Hakimu Shaidi alimuachia
mshtakiwa huyo kwa masharti ya dhamana ya mdhamini mmoja bila kusaini bondi.
Hakimu Shaidi alisema
amemuachia kwa dhamana bila bondi kwa sababu fedha zilizokamatwa zitakuwa kama
dhamana yake.Kesi imeahirishwa hadi January 18,2018.




No comments:
Post a Comment