CCM yamkabidhi kadi aliyekuwa mbunge wa Kinondoni...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu
CHAMA cha Mapinduzi(CCM) leo
kinatarajia kumpokea rasmi aliyekuwa mbunge wa Kinondoni(CUF), Maulid Mtulia.
Hatua hiyo inafuatia Mtulia juzi kujiuzulu nafasi yake hiyo pamoja na kujivua uanachama wa CUF.
Taarifa za ndani
iliyozifikia matukio360 mapema hii leo zinadai Mtulia atakabidhiwa kadi ya CCM
katika ofisi za chama hicho zilizopo
Kijitonyama kwa Alimau jijini Dar es Salaam.
" Leo(Jumatatu) majira
ya mchana, CCM inamkabidhi rasmi kadi Mtulia aliyekuwa mbunge wa
Kinondoni, tukio litafanyika katika ofisi ya chama Kijitonyama kwa Alimaua,’’
kilisema chanzo chetu cha kuaminika
ndani ya CCM
Chama cha CUF kimebariki
uamuzi wa Mtulia na kimemtakia kila la kheli.
No comments:
Post a Comment