Marekani, Korea Kaskazini wajibizana...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
MSHAURI wa masuala ya usalama
wa Ikulu ya White House nchini Marekani, HR McMaster amesema Marekani iko mbioni kukabiliana na tishio
kutoka Korea Kaskazini
Kombora la Hwasong-15 lililopaa na lenye uwezo zaidi ya makombora mengine ya Korea Kaskazini lililojaribiwa hivi karibuni
Nayo Korea Kaskazini imedai Marekani ndio inayochochea msunguano huo utakaosababisha vita .
Hata hivyo HR McMaster amesema uwezekano wa kutokea vita
unaongezeka kila siku lakini vita sio suluhu pekee, aliuambia mkutano wa
ulinzi.
Matamshi yake yanakuja siku
tatu baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lake la kwanza la kombora la
masafa marefu katika miezi miwili kinyume na vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Kombora hilo lilipaa mbali zaidi ya makombora mengine ambayo yalijaribiwa awali kabla
ya kuanguka katika bahari ya Japan.
HR McMaster ameitaka China
kuiwekea vikwazo vya mafuta taifa hilo ili kufanya kuwa vigumu kwa Pyongyang
kujaza mafuta makombora yanayofanyiwa majaribio.
Hata hivyo ikijibu mapigo Korea
Kaskazini imeishutumu Marekani kwa kuchochea vita.
Imetaja zoezi la pamoja la
kijeshi kati ya Korea kusini na Marekani kuwa la uchochezi na kwamba linaweza
kusababisha vita.
No comments:
Post a Comment