CUF Lipumba yanena Mtulia kung'atuka...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abraham Ntambara

CHAMA cha Wananchi CUF kwa upande wa wanaongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba kimechukizwa na hatua ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia  kukihama na   kujiuzulu ubunge
Mkurugeni wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF, Abdul Kambaya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Pia kinaamini mikopo isiyokuwa na tija na matumzi mabaya ya fursa za kibunge zimechangia kuzalishwa kwa madeni makubwa kwa baadhi ya wabunge  na huenda ndiyo chanzo kikubwa cha wabunge kuuza utu na heshima waliyopewa na wapiga kura wa majimbo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugeni wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF, Abdul Kambaya amesema kutokana na kitendo hicho kimeomba radhi wapiga kura wa jimbo hilo.

" CUF  kinachukua fursa hii kuwaomba radhi wapiga kura wa jimbo la Kinondoni kwa kuwaaminisha  Maulid Said  Abdallah Mtulia ni mtu makini anaweza kusimamia sera za chama na maendeleo ya wanakinondoni kwa ujumla wake," amesema.

Akizungumzia kuhusu sababu zilizomfanya Mtulia kujiunga na CCM amesema hazina mashiko.

"Kuunga mkono jitihada za rais katika kurekebisha uchumi na mambo mbalimbali sio lazima kujiondoa uanachama. Lakini hapa suala la kujiuliza ni kwamba Mtulia anamuunga mkono rais Magufuli au anaunga mkono CCM? maana kuna baadhi ya wanaccm wanapinga jitihada zinazofanywa na rais katika suala la usimamiaji wa rasilimali ". amehoji na kusema.


Kambaya amesema uamuzi wa kujiondoa kwenye chama ni utashi wake ambao hawadhani kama kuna ushawishi toka upande wa Serikali au CCM uliopelekea Mtulia kujivua uanachama.

Amesema watasimamisha mgombea mwingine katika jimbo hilo na  kuwataka wapenzi na wanachama kuwa watulivu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search